Pata taarifa kuu
DRC-UDPS-SIASA

Chama cha UDPS chaendelea kugawanyika

Chama Kikuu cha upianzani nchini DRC cha UDPS, kinasema hakina mawasiliano yeyote na Waziri Mkuu Bruno Tshibala anayesisitiza kuwa yeye ndiye Katibu Mkuu wa chama hicho na hivi karibuni, ataitisha mkutano mkuu wa cham hicho ili kumpata kiongozi mpya.

Mbele ya makao makuu ya ya chama cha upinznai cha UDPS  Kinshasa, Desemba 19, 2016.
Mbele ya makao makuu ya ya chama cha upinznai cha UDPS Kinshasa, Desemba 19, 2016. RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Mvutano umeshika kasi katika chama hicho cha upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwania mrithi wa mwenyekiti wa chama hicho Etienne Tshisekedi aliefariki miezi kadhaa iliyopita.

Kwa muda wa siku tatu Waziri mkuu wa DR Congo Bruno Tshibala pamoja na wafuasi wa chama hicho walioungana naye wanakutana katika kongamano maalum kwa ajili ya kujiandalia uchaguzi.

Hata hivyo upande mwingine wa chama hicho unaoongozwa na Felix Tshisekedi umetupilia mbali kongamano hilo na kumuita Bruno Tshibala kuwa msaliti na alijiondowa mwenyewe katika chama hicho.

Akizungumza na RFI siku ya Alhamisi, Bruno Tshibala alisema hakuna aliemfukuza katika chama hicho na kwamba bado ni katibu mkuu wa UDPS na msemaji wa Rassemblement.

Bruno Tshibala amesema chama cha UDPS sio taasisi ya jadi ambayo mtoto anamrithi baba yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.