Pata taarifa kuu
DRC-HRW-M23-USALAMA

M23 yakanusha ripoti ya Human Right Watch kuhusu wapiganaji wake

Betrand Bisimwa, kiongozi wa waasi wa zamani wa kundi la M 23 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amesema ripoti ya Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch kuwa wapiganaji wake walitumiwa na serikali ya Kinshasa, kuwakabili waandamanaji mwaka uliopita ni uongo.

wapiganaji wa kundi la zamani la M23, Februari 2014.
wapiganaji wa kundi la zamani la M23, Februari 2014. AFP PHOTO/ ISAAC KASAMANI
Matangazo ya kibiashara

Bw Bisimwa amesema wapiganaji walionekana kusajiliwa na serikali ya Kinshasa ni wale waliokuwa wameondolewa katika kundi hilo muda mrefu.

Serikali ya DRC nayo pia imekanusha ripoti hii ya Human Rughts Watch, huku Shirika hilo likisema uchaguzi wao umebaini ukweli huo baada ya kuzungumza na waasi hao wa zamani pamoja na familia zao.

Mapema wiki hii shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Right Watch lilimtuhumu rais Joseph Kabila kuwasajili wapiganaji wa zamani wa kundi la M23 kwa lengo la kuwakandamiza waandamanaji waliokuwa wakipinga utawala wake Desemba 19 na 20 mwaka 2016 jijini Kinshasa.

Kwa mujibu wa shirika hilo, ukandamizaji ulisababisha vifo vya watu 60.

Serikali ya DR Congo kupitia waziri wake wa haki za binadamu Marie Ange Mushobeka, alisema ameshangazwa na ripoti hiyo na kwamba shirika hilo halina ushahidi wowote kuhusu tuhuma hizo.

Hata hivyo Human Right Watch inasema ilikusanya ushahidi kupitia watu mbalimbali wakiwemo wapiganaji hao waliotoa ushuhuda kama anavyoeleza hapa Ida Soyere mkurugenzi wa Human Right Watch katika ukanda wa Afrika ya kati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.