Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-UCHUMI

London: Tunasikitishwa na kuchelewa kwa mazungumzo ya kujitoa katika EU

Mawaziri wa wakuu wa serikali ya Theresa May ncini Uingereza wanasikitishwa na kuchelewa kwa mazungumzo juu ya kutoka Uingereza kutoka katika Umoja wa Ulaya, lakiniwanasem abado wana uaminifu kwa Waziri wao Mkuu, amesema Waziri wa Fedha Philip Hammond.

Waziri wa Fedha wa Uingereza Philip Hammond.
Waziri wa Fedha wa Uingereza Philip Hammond. /REUTERS/Hannah McKay
Matangazo ya kibiashara

"Sisi sote tunasikitishwa na kujikokota kwa maendelo katika miezi ya hivi karibuni katika mazungumzo na Umoja wa Ulaya, ndiyo sababu Waziri Mkuu alitembelea eneo la Florence siku kumi zilizopita na alitoa hotuba ya uhakika ili kufungua mazungumzo na kuyaendeleza, "Bw Hammond amesema katika mkutano na waandishi wa habari.

Katika mji wa Manchester, ambako kunafanyika mkutano wa kila mwaka wa chama cha Conservative, Philip Hammond pia amepuuzia wigo wa mistari minne nyekundu inavyoelezwa katika vyombo vya habari vya Uingereza na Boris Johnson, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza.

"Msimamo wa Boris kuhusu masuala hayo unajulikana. Ninamuunga mkono Waziri Mkuu katika mazungumzo haya na washirika wetu wa Ulaya. Mazungumzo ambayo kwa upande mmoja ni tata na upande mwengine safi, " amesem aBw Hammond.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.