Pata taarifa kuu
UINGERZA-EU-USHIRIKIANO

Theresa May: Raia wa EU wanaendelea kupata haki sawa na Waingereza

Viongozi wa nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya walikutana mjini Brussels siku ya Alhamisi kujadili masuala yanayohusiana na kujitoa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya.

Kikao cha Baraza la Ulaya mjini Brussels Juni 22, 2017.
Kikao cha Baraza la Ulaya mjini Brussels Juni 22, 2017. REUTERS/John Thys/Pool
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May, hakushiriki katika mkutano huo. Hata hivyo, alizungumza wakati wa chakula cha jioni kabla ya mkutano wa nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya.

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amesema raia wa Umoja wa Ulaya wanaoishi nchini mwake, wanaendelea kuwa na haki sawa na raia wa nchi hiyo.

May amewaambia viongozi wenzake wa Umoja wa Ulaya jijini Brussels kuwa, hakuna atakayebaguliwa hata baada ya nchi yake kuanza kujiondoa katika Umoja huo.

Amesisitiza kuwa raia wa mataifa mengine ambao wameishi nchini Uingereza kwa zaidi ya miaka mitano, watakuwa na haki ya kupata huduma ya afya, elimu na haki zingine muhimu nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.