Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHAGUZI-LE PEN

Le Pen ajigamba mbele ya wafuasi wake Nice

Marine Le Pen, siku ya Alhamisi jioni, Aprili 27, aliendesha mkutano wake wa kwanza baada ya dura ya kwanza ya uchaguzi katika eneo la Alpes-Maritimes katika mkoa wa Nice, eneo ambako aliongoza kwa kura nyingi katika duru ya kwanza ya uchaguzi.

Marine Le Penkatika kampeni, Nice, Aprili 27, 2017.
Marine Le Penkatika kampeni, Nice, Aprili 27, 2017. REUTERS/Eric Gaillard
Matangazo ya kibiashara

Mbele ya wafuasi wake 4000, mgombea huyo wa mrengo wa kulia alitoa hotuba iliyosisimua wengi, jambo ambalo haikua kawaida yake akikemea utandawazi, uhamiaji, huku akimlenga mpinzani wake, Emmanuel Macron.

Katika mkutano huo wafuasi wake walisema wana matumaini kuwa mgombea wao atashinda katika duru ya pili ya uchaguzi. Mmoja wa wafuasi hao alisema "inabidi afanikiwe operesheni hiyo kwa chama chake sawa na mrengo anakotoka pamoja na Estrosi. "

Matakwa yake hatimaye yalitimia. Akipuuzia majina ya wanasiasa vigogo walioungana na Emmanuel Macron, mgombea wa mrengo wa kulia alimshambulia kiongozi wa LR wa mkoa wa Provence-Alpes-Côte d'Azur (PACA), meya wa zamani wa mkoa wa Nice. "Robert Hue, Manuel Valls na Christian Estrosi . "Meya wa zamani wa mkoa wa Nice alizomelewa na wafuasi wake wa Le Pen waliohudhuria mkutano huo.

Hata hivyo Marine Le Pen amekua akilaani utaratibu wa mapokezi kwa wahamiaji, huku akibaini kwamba hatokubali nchi yake kuendelekukabiliwa na hali hiyo iwapo atachaguliwa kuwa rais wa Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.