Pata taarifa kuu
UFARANSA-MACRON-SIASA

François Hollande kumpigia kura Emmanuel Macron

Siku moja baada ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini Ufaransa, Rais François Hollande alitangaza siku ya Jumatatu, April 24 wakati hotuba iliyorushwa kwenye televisheni kwamba atampigia kura Emmanuel Macron Mei 7 katika duru ya pili, ambapo atapambana na mgombea wa chama cha FN, Marine Le Pen.

François Hollande atangaza kwamba atampigia kura Emmanuel Macron, Aprili 24, 2017.
François Hollande atangaza kwamba atampigia kura Emmanuel Macron, Aprili 24, 2017. FRANCE TELEVISIONS POOL via REUTERS TV
Matangazo ya kibiashara

François Hollande aliahidi jioni ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais kwamba ataeleza msimamo wake mapema wiki hii. Ahadi ambayo hatimaye imetekelezwa. Katika taarifa kutoka Ikulu ya Elysee siku ya Jumatatu mchana, rais Hollande alitangaza kuwa atampigia kura Emmanuel Macron, dhidi ya kile alichokiita "hatari" kwa Ufaransa ambayo itasababishwa na ushindi wa Marine Le Pen tarehe 7 Mei.

"Uwepo wa mrengo wa kulia inasababisha kwa mara nyingine kukabiliwa na hatari kwa nchi yetu," alisema François Hollande. Kwa mujibu wa rais Hollande, ushindi wa mgombea wa chama cha FN na kutoka kwa Euro ambavyo aaliahidi kutasababisha hali ngumu ya ya maisha na manunuzi kwa wananchi wa Ufaransa, wakati ambapo "hatua za udhibiti" zinanaweza kusababisha ajira nyingi kufutwa. "Kwa hiyo kuna hatari ya kutengwa kwa Ufaransa, lakini pia kuvunjika kwa uhusiano na Umoja wa Ulaya," ameonya François Hollande. "Kutokana na na hatari hizo, haiwezekani kuwa kimya, " rais Hollande amesema.

Kwa mujibu wa matokeo ya mwisho ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini Ufaransa yaliyotangazwa na Wizara ya Mambo ya Ndani, mgombea wa En Marche!, Emmanuel macron, amemshinda Marine Le Pen aliyepata 21.30% ya kura. François Fillon amechukua nafasi ya tatu akipata 20.01%, huku Jean-Luc Mélenchon akichukua nafasi ya kwa 19.58% ya kura.

Emmanuel Macron atapambana baada ya wiiki mbili katika duru ya pili na Marine le Pen ambae ni mgombea wa chama chenye mrengo wa kulia cha National Front.

Macron mwenye umri wa miaka thelathini na tisa na aliyewahi kuwekeza katika sekta ya benki, hajawahi kuingia katika kinyang'anyiro cha uchaguzi kabla, amesema, shaka, hofu na hamu ya mabadiliko aliyokumbana nayo katika kampeni ndio iliyosababisha wapiga kura kuacha vyama vikuu vya kisiasa ambavyo vimekuwepo uongozini kwa miaka thelathini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.