Pata taarifa kuu
UFARANSA-SIASA

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa, Bruno Le Roux, atangaza kujiuzulu

Ofisi ya mashitaka mjini Paris imetangaza kumchunguza Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Ufaransa Bruno Le Roux baada ya madai kuwa, aliwaajiri mabinti wake wawili kama wasaidizi wake alipokuwa mbunge.

Bruno Le Roux Desemba 22, 2016.
Bruno Le Roux Desemba 22, 2016. REUTERS/Charles Platiau/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Bw Le Roux baada ya kupokelewa na rais wa Ufaransa François Hollande ena Bernard Cazeneuve, alitangaza kujiuzulu kwenye nafasi yake aliyokua akishikilia kwa kipindi kisichozidi miezi minne. Katibu Dola Matthias Fekl ameteuliwa kuchukua nafasi yake.

Le Roux mwenye umri wa miaka 51, anakutana na Waziri Mkuu Bernard Cazeneuve baadaye sikuy ya Jumanne, kujieleza kuhusu madai haya.

Kituo cha Habari cha TMC, kimeripoti kuwa Le Roux wakati akiwa Mhunge aliwaajiri mabinti wake kati ya mwaka 2009 na 2016 na kuwalipa Dola za Marekani 59,000.

Madai haya yamewakumbusha raia wa Ufaransa kuhusu Francois Fillon mgombea urais nchini humo kupitia chama cha Republican ambaye pia amedaiwa.

Licha ya madai haya, sheria nchini Ufaransa inawaruhusu wabunge kuwaajiri watu wa Familia zao ikiwa watafanya kazi itakayotambuliwa.

Hata hivyo, Fillion na sasa Le Roux kutoka chama cha Kisosholisti wanadaiwa kutoa ajira hizo lakini watu wao wa Familia hawakufanya kazi kama ilivyodaiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.