Pata taarifa kuu
DRC-MAZUNGUMZO-SIASA

Serikali ya DRC na upinzani kujadili juu utekelezaji wa Mkataba wa Disemba 31

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, serikali na upinzani wanatazamiwa kukutana Jumanne hii ili kufafanua sheria za utekelezaji wa mkataba uliosainiwa tarehe 31 Desemba 2016.

Chama cah MLC kinalaani Etienne Tshisekedi kuwaa Mwenyekiti wa CNSAP, DRC.
Chama cah MLC kinalaani Etienne Tshisekedi kuwaa Mwenyekiti wa CNSAP, DRC. THIERRY CHARLIER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Siku tatu baada ya makubaliano ya kihistoria ya Desemba 31, "mkutano wa kwanza unatazamiwa kufanyika Jumanne hii katika hali ya kuweka sawa sheria za utekelezaji wa Mkataba uliyosainiwa hivi karibuni kati ya serikali na upinzani," amesema Kasisi Donatien Nshole, msemaji wa Baraza kuu la Maaskofu nchiniCongo (Cenco). Mkataba huu unamruhusu rais Joseph Kabila kubaki madarakani mpaka uchaguzi wa mrithi wake ifikapo mwishoni mwa mwezi Desemba 2017.

"Mkataba tayari umeanza kufanya tangu iliposainiwa, tulikubaliana kujadili mpango maalum kuhusu muundo wa Baraza la kitaifa la ufuatiliaji wa mkataba na mchakato wa uchaguzi (CNSAP), mfumo wa uteuzi wa wajumbe 28 wa taasisi hiyo na uundwaji wa serikali ya mpito, " amethibitisha Christophe Lutundula, mmoja wa waliosaini makubaliano kwa niaba ya muungano wa vyama vya upinzani wa Rassemblement unaoongozwa na Etienne Tshisekedi.

Saini kumi bado zinakosa

Hayo yakijiri inaarifiwa kuwa kwenye mkataba huo bado kunakosa saini za wajumbe kumi wa upinzani ambao hawajasaini kwenye waraka huo.Wajumbe hao ni kutoka chama cha MLC cha aliyekuwa Makamu wa rais Jean-Pierre Bemba, ambaye kwa sasa anazuiliwa katika mjini Hague kwa uhalifu dhidi ya binadamu, na baadhi ya wajumbe kutoka vyama vya upinzani vyenye wafuasi wadogo walioshiriki katika mazungumzohayo

Wakati wa mazungumzo, chama cha MLC kiliomba kipewa nafasi ya Mwenyekiti wa Baraza la kitaifa la ufuatiliaji wa mkataba na mchakato wa uchaguzi (CNSAP), kikilaani uteuzi wa Etienne Tshisekedi kwenye nafasi hiyo na nafasi ya Waziri mkuu wa mpito pia kutoka muungano wa upinzani wa Rassemblement.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.