Pata taarifa kuu
GAMBIA-UCHAGUZI

Raia wa Gambia wanapiga kura kumchagua rais

Uchaguzi wa urais unafanyika Alhamisi hii nchini Gambia. Kinyanganyiro ni kati ya rais Yahya Jammeh ambaye ameongoeza nchi hiyo kwa miaka 22 sasa, na mpinzani wa pekee, Adama Barrow.

Bango la kampeni ya Rais Yahya Jammeh katika mji wa Banjul, mji mkuu wa Gambia, Novemba 22, 2011.
Bango la kampeni ya Rais Yahya Jammeh katika mji wa Banjul, mji mkuu wa Gambia, Novemba 22, 2011. AFP PHOTO / SEYLLOU
Matangazo ya kibiashara

Wadadisi wa siasa nchini Gambia wamesema kwa mara ya kwanza huenda rais Jammeh ambaye baadhi ya raia wa Gambia wanasema ni dikteta, akapata upinzani mkali kutoka kwa Barrow.

Waangalizi wa Umoja wa Ulaya walinyimwa vibali vya kwenda kushuhudia uchaguzi huu.

Inaarifiwa kuwa vyama saba vimeamua kuunganisha nguvu zao na kumpa kibali mgombea mmoja Adama Barrow ambaye anatafsiriwa kama tishio kwa Rais Yahya Jammeh.

Pamoja na hayo yote rais Jammeh amejinasibu kuwa hatishwi na jambo lolote katika uchaguzi huo wakati huo huo wapinzani wake wanadai tabia zisizofaa zimemuandama rais huyo miezi kadhaa iliyopita kabla ya kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho.

Mpaka sasa inaarifiwa kuwa serikali ya Gambia imekata mawasiliano yote ya simu ikiwemo mitandao huku wapinzani wakichelea mchezo mchafu kufanywa ikiwemo uvunjifu wa amani kwa hatua hiyo ya serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.