Pata taarifa kuu
MAREKANI-GAMBIA-MAPINDUZI-SIASA

Wamarekani 2 wakamatwa kufuatia jaribio la mapinduzi Gambia

Wizara ya sheria ya Marekani imewafungulia mashitaka raia wawili wa Marekani wenye asili ya Gambia wakituhumiwa kupanga jaribio la mapinduzi lililofeli Desemba 30 mwaka 2014 nchini Gambia.

Rais wa Gambia Yahya Jammeh, Juni 23 mwaka 2014, wakati wa ziara yake nchini Guinea-Bissau.
Rais wa Gambia Yahya Jammeh, Juni 23 mwaka 2014, wakati wa ziara yake nchini Guinea-Bissau. AFP PHOTO / ALFA BA
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Waziri wa Sheria, Eric Holder, Cherno Njie, mwenye umri wa miaka 57 na Papa Faal, mwenye umri wa miaka 46 " walipanga njama ya kuipindua serikali ya kigeni kupitia vurugu kwa kukiuka sheria ya Marekani".

Kwa mujibu wa Idara ya Ujasusi ya Marekani FBI, watu hao wawili walinunua hivi karibuni silaha na vifaa vya kijeshi ambavyo vilisafirishwa nchini Gambia wakiwa na nia yakumtimua madarakani rais Jammeh, wakiwa na imani kuwa sehemu hiyo ya msaada itasaidia kwa kiwango kikubwa kuuangusha utawala wa Yahya Jammeh.

Lakini wakati walishambulia Ikulu ya rais Desemba 30 walizidiwa nguvu na kurudishwa nyuma na jeshi linalomuunga mkono rais Jammeh ambaye wakati huo alikuwa ziarani nje ya nchi.

Papa Faal na Cherno Njie walifaulu kutoroka na kurudi Marekani ambapo walikamatwa walipowasili mjini Washington. Mmoja alikamatwa Januari 1, mwengine Januari 3. Cherno Njie ni mfanyabiashara anayeishi katika mji wa Texas, ambaye anadaiwa kufadhili jaribio hilo la mapinduzi. Lengo lake ilikua kurejesha demokrasia nchini Gambia.

Papa Faal kwa upande wake, amesema kwamba alivutiwa na wazo la kuupindua utawala wa rais Jammeh kwa sababu aliiba kura wakati wa uchaguzi. Faal alihudumu miaka kadhaa katika Jeshi la Marekani na aliwahi kutumwa nchini Afghanistan. Papa Faal na Cherno Njie wanakabiliwa na kifungo cha miaka 25 jela.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.