Pata taarifa kuu
KOREA KUSINI-SIASA

Rais wa Korea Kusini mbioni kujiuzulu

Rais wa Korea Kusini Park Geun-hye amesema yuko tayari kujiuzulu lakini ameliomba bunge la nchi hiyo kutafuta njia ya kumuwezesha kuondoka madarakani, baada ya kukumbwa na kashfa ya ufisadi.

Rais wa Korea Kusini, Park Geun-Hye, akilihutubia taifa, katika Ikulu ya Blue House mjini Seoul, Korea Kusini,Novemba 29, 2016.
Rais wa Korea Kusini, Park Geun-Hye, akilihutubia taifa, katika Ikulu ya Blue House mjini Seoul, Korea Kusini,Novemba 29, 2016. REUTERS/Jeon Heon-Kyun/Pool
Matangazo ya kibiashara

Park Geun-hye amesema ataachia "bunge kila kitu kuhusu mustakabali wake, ikiwemo kufupisha muhula wake", lakini hataki kuacha pengo uongozini.

Bi Park amekabiliwa na shinikizo za kumtaka ang'atuke huku uchunguzi wa iwapo alimruhusu rafiki yake ya muda mrefu kuwa na usemi kuhusu uamuzi wa kisiasa kwa manufaa yake binafsi ukiendelea.

Amesema anataka bunge limsaidie kupata njia bora zaidi ya kuondoka madarakani bila kuacha pengo au kuzua mzozo wa kisiasa.

Baadhi ya viongozi katika chama tawala walikuwa wamesema alifaa kung'atuka "kwa heshima" kabla ya mambo kufikia hatua ya sasa.

Bunge lilikuwa limepangiwa kujadili iwapo anafaa kuondolewa madarakani Ijumaa.

Vyama vya upinzani sasa vimemtuhumu Park Geun-hye kwa kujaribu kuchelewesha mpango wa bunge kumuondoa madarakani.

Hata hivyo kiongozi huyo ameomba msamaha mara mbili na kusema amesikitishwa sana na mzozo wa kisiasa ambao unamkabililichja ya kukataa kuondoka mamlakani.

Waendesha mashtaka nchini Korea Kusini, walisem akuwa waligundua kwamba Rais Park Guen Hye, alihusika na kashfa ya ubadhirifu wa pesa za umma inayomkabili rafiki yake wa mda mrefu Choi Sun-Sil.

Wanasema hawana uwezo wa kumfungulia mashtaka rais huyo kwa sababu analindwa na katiba lakini wataendelea kumchunguza.

Bi Choi, anatuhumiwa kwa kutumia usuhuba wake na rais Guen Hye, kuingilia masuala ya uongozi wa taifa hilo, ambapo aliwaamuru wakurugenzi wa mashirika makubwa, kuchangia mamilioni ya pesa wakfu ambao ana uendesha yeye binafsi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.