Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-ZUMA

Rais Jacob Zuma kukutana na maveterani wa ANC

Nchini Afrika Kusini, Rais Jacob Zuma anatazamiwa kukutana Jumatatu hii Novemba 21 na wawakilishi wa maveterani wa ANC, wanaoomba rais Zuma ajiuzulu na kuomba mkutano wa chama ili kumchagua kiongozi mpya wa chama cha ANC.

Jacob Zuma, hapa mbele ya Bunge mjini Cape Town, Machi 17, 2016.
Jacob Zuma, hapa mbele ya Bunge mjini Cape Town, Machi 17, 2016. REUTERS/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Maveterani 101, ikiwa ni pamoja na Ahmed Kathrada au Waziri wa zamani wa Fedha, Trevor Manuel, wamejiunga katika wito huu. Wanadai tangu mwezi Septemba mkutano na Rais wa Afrika Kusini. Wanataka kuuliza vizurikuhusu kesi mbalimbali zinazochafua hali ya kisiasa ya Afrika Kusini. mkutano unaonekana kuwa utakua na mvutano. Rais Jacob Zuma anaonekana kuwa mkali kutokana na kauli zake ambazo zilikosolewa wakati wa hotuba ya mwishoni mwa wiki.

Msemaji wa wa chama cha ANC amesem akuwa Rais Jacob Zuma atakutana mwenyee na maveterani wa chama. Maveterani hawa wanahitaji kuzunumzia matokeo mabaya ya cham acha ANC katika uchaguzi wa mikoa, lakini pia wanataka kujadili matukio ya hivi karibuni yanayouchafua uongozi wa rais Jacob Zuma.

Katika mkutano huu, maveterani watawasilisha waraka ulio na kichwa cha habari 'hatima yetu', utakaowakusanya makarani wao na madai yao kwa minajili ya ufunguzi wa 'mjadala wenye kujenga' kwa mustakabali wa chama.

Mwishoni mwa juma hili Rais Zuma aliwakosoa wapinzani wake akiwataja kuwa ni "vibaraka" wanaotumiwa na "adui kutoka nje" na nchi za Magharibi, " alisema.

"Kuna baadhi ya wale ambao sijaona tangu mwaka 1994," amesisitiza rais Jacob Zuma. "Watu hao wamekua wakikurupuka na kuzungumza kwenye vyombo vya habari badala ya kutumia miundo ya chama," Ras Zuma amesema tena na kushutumu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.