Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-SIASA-UFISADI

Bunge lakataa kupiga kura ya kutokuwa na imani dhidi ya Zuma

Bunge la Afrika Kusini limefutilia mbali Alhamisi hii kura ya pendekezo la kupiga kura ya kutokua na imani dhidi ya Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma licha ya madai ya hivi karibuni ya ufisadi.

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akabiliwa na tuhuma za ufisadi.
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akabiliwa na tuhuma za ufisadi. REUTERS/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Uchunguzi uliofanywa na tume ya kukabiliana na ufisadi nchini Afrika Kusini ulisema kuwa jopo la majaji linafaa kubuniwa ili kuchunguza madai ya uhalifu katika serikali ya Zuma.

Uchunguzi huo ulipata ushahidi kwamba familia ya Gupta ilio na uhusiano mkubwa na rais Zuma huenda ilikuwa na ushawishi mkubwa katika uteuzi wa baraza la mawaziri.

Uchunguzi wa tume ya kukabiliana na ufisadi nchini humo wiki iliopita ulizua madai ya utovu wa nidhamu dhidi ya Rais Jacob Zuma.

Chama cha Rais Zuma ANC kina wabunge wengi katika bunge na mswada huo wa upinzani ulishindwa kwa kura 214 dhidi ya 126.

Hii ni kura ya tatu ya kutokuwa na imani naye iliowasilishwa bungeni katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.