Pata taarifa kuu
MALI-UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi wa mikoa wafanyika nchini Mali chini ya mvutano

Wananchi wa Mali wamepiga kura Jumapili hii Novemba 20 kwa uchaguzi wa mikoa, hatua ya kwanza tangu uchaguzi wa rais Ibrahim Boubacar Keïta mwaka 2013, pamoja na kiwango cha ushiriki ambacho kimetangazwa kuwa cha chini kabisa, kwa sababu ya kukosekana kwa utulivu katika nchi hii iliyo chini ya hali ya dharura.

Mpiga kura katika moja ya vituo vya kupigia kura, lakini katika baadhi ya maeneo ya chi ya Mali, wapiga kura hawakuweza kwenda kupiga kura kwa uchaguzi wa miko, Jumapili hii Novemba 20, 2016.
Mpiga kura katika moja ya vituo vya kupigia kura, lakini katika baadhi ya maeneo ya chi ya Mali, wapiga kura hawakuweza kwenda kupiga kura kwa uchaguzi wa miko, Jumapili hii Novemba 20, 2016. REUTERS/Adama Diarra
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huu, ambao kiwancgo cha ushiriki kilikua hakijajulikana hadi saa sita mchana umefanyika sanjari na maadhimisho ya kwanza ya mashambulizi ya wanajihadi dhidi ya hoteli Radisson Blu mjini Bamako, ambapo watu 20 waliuawa, ikiwa nin pamoja na washambuliaji wawili.

"Uchaguzi huu uliahirishwa mara nne. Hiyo inatosha, "amesema rais Keita baada ya kupiga kura, huku akipongeza 'zoezi la kidemokrasia. '

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon siku ya Jumamosi alitoa wito kwa serikali, upinzani na makundi yaliyosaini mkataba wa amani wa mwezi Mei hadi Juni 2015 "kuhakikisha uchaguzi unafanyika, bila vurugu, ambapo hali ya kisiasa na usalama imekua ikiruhusu kufanyika kwa uchaguzi huo. "

Kwa kutambua kuwa 'ucheleweshaji mkubwa katika utekelezaji wa masharti muhimu ya mkataba', ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa mamlaka ya muda katika eneo la Kaskazini, na 'hali ya usalama katika eneo la kaskazini na baadhi ya maeneo ya kati mwa nchi vinaweza kuhatarisha maandalizi ya uchaguzi ', Ban Ki-moon alitoa wito kwa serikali" kupunguza mvutano "ambao unaweza kusababisha hali hiyo.

Chanzo cha utawala kimebaini kwamba hali ya sintofahamu imeripotiwa katika mji mkuu wa nchi hii, Bamako na katikati mwa nchi.

Zoezi la kupiga kura halikufanyika katikajimbo la Kidal, kaskazini-mashariki mwa nchi, ngome ya kundi la waasi la Azawad.

Katika jimbo jirani la Gao, uchaguzi umefanyika katika baadhi ya wilaya.

Katika jimbo la Timbuktu, kaskazini-magharibi mwa nchi, ambapo vifaa vya uchaguzi viliondolewa na kuchomwa moto wakati mashambulizi tofauti, ikiwa ni pamoja na Jumapili. Kama uchaguzi ulifanyaka kwa hali ya utulivu katika mji wa jimbo hilo, katika maeneo mengine kuliripotiwa vurugu na pia haukufanyika katika baadhi ya maeneo ya jimbo hilo.

"Watu hawakujitokeza kwa wingi. Kulikuwa na wasiwasi, lakini wote hali ni nzuri mpaka sasa, " Oumar Moussa capita Sareykeyna, mtuu maarufu katika jimbo la Timbuktu, ameliambia shirika la habari la AFP.

Itafahamika kwamba mgombea wa chama kidogo cha upinzani alitekwa nyara siku ya Jumamosi asubuhi katika eneo la Koro, katikati mwa nchi, amesema kiongozi wa chama cha mgombea huyo, Mamadou Sidibé, akiongeza kuwa "gari la Saibou Barry lilichomwa moto na yeye mwenyewe alipelekwa katika eneo lisilojulikana. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.