Pata taarifa kuu
MALI-TUMBUKTU

Wananchi wa Mali watofautiana kuhusu hukumu dhidi ya Ahmad al-Faqi al-Mahdi

Wananchi wa Mali wametofautiana kuhusu hukumu ya miaka tisa iliotolewa na Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC dhidi ya mbabe wa kivita Ahmad al-Faqi al-Mahdi baada ya kukutwa na hatia ya makosa 9 ya ubomoaji wa makaburi ya zamani na Miskiti.

Ahmad al-Faqi al-Mahdi aliyekukutwa na hatia ya makosa 9 ya ubomoaji wa makaburi ya zamani na Miskiti, nchini Mali..
Ahmad al-Faqi al-Mahdi aliyekukutwa na hatia ya makosa 9 ya ubomoaji wa makaburi ya zamani na Miskiti, nchini Mali.. REUTERS/Patrick Post/Pool
Matangazo ya kibiashara

Hukumu hiyo haikushutuwa wengi kwani mtuhumiwa alitakiwa amekiri makosa yake na kushirikiana kikamilifu na majaji wa mahakama ili kupunguziwa adhabu kati ya miaka 9 na 11 badala ya miaka 30.

Meya wa jiji la Tombuktu Hallé Ousmane amepongeza hukumu hiyo na kuonya wale wote ambao bado wanatekeleza makosa ya aina hiyo.

Hata hivyo shirika la kimataifa linalotetea haki za binadamu FIDH na shirika la haki za binadamu nchini Mali yamesikitishwa na hukumu hiyo ambayo haikugusa makosa ya uhalifu wa kibinadamu ambayo yalitekelezwa na Al Mahdi wakati akiwa kiongozi wa wanamgambo wakati wa matukio hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.