Pata taarifa kuu
MAREKANI-SIASA-UCHAGUZI

Barack Obama katika kampeni kumuokoa Hillary Clinton

Ikiwa zimesalia siiku tano kabla ya uchaguzi wa urais nchini Marekani, utafiti unaonyesha kuwa Hillary Clinton na Donald Trump wameendelea kukaribiana sana. Utafiti wa hivi karibuni unampa Donald Trump ushindi katika majimbo kadhaa muhimu. Hali hiyo ndio imepelekea Barack Obama kuamua kumfanyia kampeni Waziri wake wa zamani wa Mashauriano ya Kigeni.

Barack Obama katika jimbo la North Carolina, akifanya kampeni kwa niaba ya Hillary Clinton, Novemba 2, 2016.
Barack Obama katika jimbo la North Carolina, akifanya kampeni kwa niaba ya Hillary Clinton, Novemba 2, 2016. REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Mwaka 2008, 90% ya wapiga kura weusi walimpigia kura Barack Obama. Miaka minane baadaye, Wamarekani weusi hawajahamasishwa vya kutosha kwa kumpigia kura Bi. Hillary Clinto ambaye anataka kumrithi rais anayemaliza muda wake.

Kwa muda wa siku tano zinazosalia, rais anayemaliza muda wake atakua akifanya kampeni katika majimbo ya North Carolina, Ohio na Florida, jambo ambalo si la kawaida katika kampeni ya urais. Na Rais Barack Obama ameweka matumaini yake makubwa kwa Wamarekani weusi.

Jumatano, Novemba 2, Obama alikuwa alialikwa na Tom Joyner katika kipindi cha Morning Show kinachorushwa kwenye radio kila siku asubuhi, ambpo walishiriki kwa kiasi kikubwa Wamarekani weusi. "Kura za Wamarekani weusi si imara kama ambavyo inelipaswa kuwa. Najua kuwa watu wengi katika vinyozi, katika maduka ya vipodozi au katika vitongoji wanakoishi Wamarekani weusi wanampenda Barack. Wanampenda Michelle. Lakini unajua nini? Kila mmoja wenu anapaswa kuelewa kwamba kila kitu ambacho tumeweza kufanya kinategemea sasa na uwezo wangu wa kumkabidhi mwenge mtu ambaye anafuata viwango sawa na mimi, " amesema Rais Barack Obama.

Kwa hiyo Barack Obama hamfanyii kampeni Hillary Clinton. Lakini pia anajaribu kuokoa urithi wake wa kisiasa ambao Donald Trump amekwisha kuahidi kuuondoa atakapopata ushindi.

■ Uchunguzi barua pepe: Obama aonyesha msimamo wake

Rais wa Marekani Barack Obama ameonya kuwa uchunguzi wa shirika la kijasusi la FBI kuhusu barua pepe za Hillary Clinton usiendeshwe kwa njama za kumuangusha wala za kumkashifu.

Maneno ya Obama yanaonekana kama ukosoaji ambao si wa moja kwa moja kwa mkurugenzi wa shirika la upelelezi la FBI, James Comey. James Comey alitangaza wiki iliyopita kuwa shirika hilo limeanza tena uchunguzi baada ya kupokea barua pepe ambazo zinaweza kuwa za muhimu.

Obama amemwaambia waandishi wa Marekani kwamba anaimani kamili juu ya mgombea urais wa Democratic.

Bw. Obama ambaye amekuwa katika jimbo la North Carolina kumpigia debe Bi.Clinton, ameonya kuwa hatima ya Marekani na dunia ipo hatarini ikiwa Trump atachaguliwa.

Rais wa Marekani Barrack Obama amewataka wafuasi wa chama cha Democratic kujitokeza kwa wingi na kumpigia kura Hillary Clinton.

Trump naye akiwa katika jimbo la Florida, amemtaka rais Obama kuacha kumfanyia kampeni Bi.Clinton na badala yake kuongoza nchi .

Uchaguzi wa Marekani ni Jumanne wiki ijayo lakini tayari kura za mapema zimeanza kupigwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.