Pata taarifa kuu
USA-CLINTON-UCHAGUZI-MAREKANI

Clinton aitaka FBI kutoa maelezo mapema kuhusu uchunguzi mpya inaoufanya

Mgombea urais wa chama cha Democrat nchini Marekani, Hillary Clinton, amelitaka shirika la ujasusi nchinik humo, FBI, kueleza bila kuchelewa sababu za wao kufungua tena uchunguzi kuhusu matumizi ya barua pepe zake binafsi.

Hillary Clinton, mgombea wa Democrat, October 28, 2016.
Hillary Clinton, mgombea wa Democrat, October 28, 2016. REUTERS/Brian Snyder
Matangazo ya kibiashara

Wananchi wa Marekani "wanastahili kupata ukweli ulio kamili na ushahidi wa kutosha haraka sana," alisema Hillary Clinton.

FBI inasema kuwa kwa sasa wanazo barua pepe mpya zinazohusiana na matumizi binafsi ya barua pepe yake wakati alipokuwa waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani.

Akiwahutubia wafuasi wake, mgombea wa Republican, Donald Trump, amesema kuwa uchunguzi huu kufufuliwa siku 11 kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu, ni kashfa kubwa zaidi kuliko hata ile ya Watergate.

Barua pepe hizi mpya ni sehemu ya uchunguzi tofauti kabisa na ule wa awali, ambao unafanywa dhidi ya watu waliokuwa karibu na mume wake, Bill Clinton, Huma Abedin.

Simu za Huma na Anthony Weiner zilizuiliwa na maofisa wa FBI kwa uchunguzi zaidi, kubaini ikiwa walizitumia kutuma ujumbe wa kimapenzi kwa msichana mmoja mwenye umri wa miaka 15 mjini North Carolina.

Uvumbuzi wa barua pepe hizi mpya, ulioneshwa katika barua mpya kwa baraza la Congrees, iliyoandikwa na mkurugenzi wa FBI, James Comey.

Hata hivyo Comey hakuweka wazi ikiwa barua pepe mpya zilizopatikana zinaweza kuwa muhimu au la, lakini akasisitiza kuwa FBI inachunguza barua ambazo ziliandikwa na watu hao.

Clinton mwenyewe amesema kuwa ana amini uchunguzi huu unaoendelea kufanywa na FBI, hautabadili kitu chochote kuhusu maamuzi yaliyokuwa yamefikiwa mwezi Julai mwaka huu, ambapo alimsafisha Clinton dhidi ya makosa ya jinai, licha ya kukiri kuwa alifanya uzembe mkubwa kutumia mawasiliano binafsi.

FBI iliahirisha mpango wake wa kumshtaki Clinton kutokana na kutumia barua pepe binafsi wakati akiwa waziri wa mambo ya kigeni kati ya mwaka 2009 na 2013.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.