Pata taarifa kuu

Mwanasheria Mkuu wa serikali atangaza kuachana na shutma zinazomkabili Waziri wa Fedha

Waziri wa Fedha Pravin Gordhan alikuwa anatuhumiwa kosa la udanganyifu wakati alipokua akiongoza mamlaka ya kodi ya Afrika Kusini. Kesi hii iliibua mvutano wa kisiasa ndani ya serikali. Bw Gordhan alikua anatazamiwa kusikilizwa mahakamani Novemba 2.

Waziri wa Fedha wa Afrika Kusini, Pravin Gordhan, akijitetea mbele ya Bunge mjini Cap, Oktoba 26, 2016.
Waziri wa Fedha wa Afrika Kusini, Pravin Gordhan, akijitetea mbele ya Bunge mjini Cap, Oktoba 26, 2016. REUTERS/Sumaya Hisham
Matangazo ya kibiashara

Shinikizo limekuwa likiendelea kuongezeka mahakamani katika kesi dhidi ya Waziri wa Fedha Pravin Gordhan. Awali licha ya uvumi, ofisi ya mwendesha mashitaka ilikanusha kuwa imeachana na kesi hiyo, huku msemaji wa Mwendesha mashitaka Mkuu akisema kuwa taarifa hiyo ni uongo na uzushi mtupu.

Huu ni "uongo na ni habari zisizo kuwa na msingi", kwa mujibu wa msemaji wa Mwendesha mashitaka Mkuu wa jamhuri. "Hii haina maana," amesisitiza. Hata hivyo amesema kuwa Shaun Abrahams anaendelea kuchunguza kesi hii na anahitaji "muda wa kutosha ili achukuwe maamuzi".

Waziri Pravin Gordhan alikua anatazamiwa kusikilizwa mahakamani Jumatano Novemba 2.

Mashtaka dhidi yake yaliibua hali ya sintofahamu katika chama tawala cha ANC.

Ofisi ya mashitaka imekua ikikosolewa na baadhi ya wanasiasa. Viongozi 80 wa makampuni wameamua kumtetea Waziri wa Fedha ambaye anaungwa mkono na wajumbe kadhaa wa serikali, na vigogo wa kihistoria wa chama cha ANC.

Chama cha Democratic Alliance kilisema mwishoni mwa wiki hii iliyopita kwamba "jambo pekee la kufanya kwa Shaun Abrahams ni kuachana na mashtaka na kujiuzulu." Mawakili wa Pravin Gordhan wamebaini kwamba kesi imechochewa kisiasa, na kwamba upande wa mashtaka hauna ushahidi wa kutosha dhidi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.