Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-SHERIA

Waziri wa Fedha Pravin Gordhan kufikishwa mahakamani

Nchini Afrika Kusini, shinikizo limeendelea kuongezeka mahakamani katika kesi dhidi ya Waziri wa Fedha Pravin Gordhan, anayekabiliwa na kosa la udanganyifu. Licha ya uvumi, ofisi ya mwendesha mashitaka imekanusha kuwa imeachana na kesi hiyo. Lakini kesi hii bado ipo katika ngazi ya" uchunguzi", siku chache kabla ya kusikilizwa kwa Waziri wa Fedha na mahakama Jumatano Novemba 2.

Waziri wa Fedha wa Afrika Kusini Pravin Gordhan, Machi 14, 2016.
Waziri wa Fedha wa Afrika Kusini Pravin Gordhan, Machi 14, 2016. REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Wiki hii inayoanza ni yenye maamuzi kwa Waziri wa Fedha Pravin Gordhan. Mwishoni mwa wiki hii iliyopita, vyombo vya habari nchini Afrika Kusini viliripoti kuwa Mwrendesha mashitaka Mkuu wa jamhuri Shaun Abrahams aliandika barua akisema kuwa ameachana na mashtaka dhidi ya Waziri wa Fedha.

Taarifa hii imekanushwa saa chache baadaye. Huu ni "uongo na ni habari zisizo kuwa na msingi", kwa mujibu wa msemaji wa Mwendesha mashitaka Mkuu wa jamhuri. "Hii haina maana," amesisitiza. Hata hivyo amesema kuwa Shaun Abrahams anaendelea kuchunguza kesi hii na anahitaji "muda wa kutosha ili achukuwe maamuzi".

Hata hivyo Pravin Gordhan anatazamiwa kusikilizwa na mahakama Jumatano Novemba 2. Mashtaka dhidi yake yaliibua hali ya sintofahamu katika chama tawala cha ANC.

Ofisi ya mashitaka imekua ikikosolewa na baadhi ya wanasiasa. Viongozi 80 wa makampuni wameamua kumtetea Waziri wa Fedha ambaye anaungwa mkono na wajumbe kadhaa wa serikali, na vigogo wa kihistoria wa chama cha ANC.

Chama cha Democratic Alliance kilisema mwishoni mwa wiki hii iliyopita kwamba "jambo pekee la kufanya kwa Shaun Abrahams ni kuachana na mashtaka na kujiuzulu." Mawakili wa Pravin Gordhan wamebaini kwamba kesi imechochewa kisiasa, na kwamba upande wa mashtaka hauna ushahidi wa kutosha dhidi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.