Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA

Wito wa kusalia nyumbani waitikiwa mjini Kinshasa

Siku moja baada ya kusainiwa kwa mkataba wa kisiasa kati vyama vinavyounga mkono serikali na baadhi ya vyama vya upinzani, makundi mengine ya upinzani yamewatolea wito raia wa DR Congo kusalia nyumbani Jumatano hii, Oktoba 19 ili kumpa onyo kwa kadi ya manjano Rais Joseph Kabila. Wito huo umeitikiwa kwa kiasi kikubwa mjini Kinshasa, ingawa katika baadhi ya maeneo, shughuli zimekua zikiendelea.

Mtaa wa kibiashara Jumatano hii asubuhi, moja ya maeneo makuu ya kibiashara ya mji mkuu wa DR Congo, Kinshasa.
Mtaa wa kibiashara Jumatano hii asubuhi, moja ya maeneo makuu ya kibiashara ya mji mkuu wa DR Congo, Kinshasa. Sonia Rolley/RFI
Matangazo ya kibiashara

Jumatano hii asubuhi, mitaa ilikua patupu, maduka pamoja na shule vilifungwa, magari hayakua barabarani na msongamano wa magari haukuwepo Jumatano hii katika baadhi ya maeneo kunaonekana msongamano mkubwa wa magari. Mabasi ya serikali yalikua yakiegesha kila mahali kwa kusubiri wafanyakazi.

Hata hivyo baadhi ya waendesha pikipiki za uchukuzi na baadhi ya wachuuzi wa mitaani walionekana katika maeneo mbalimbali wakiendesha shughuli zao. Lakini watu hao wamesema kuwa wanaunga mkono wito huo lakini kutokana na hali ya maisha inayowakabili wameamua kuendesha shughuli zao kama kawaida "Njaa hukusababisha kufanya jambo ambalo haukulitaraji kulifanya," amesema mfanyabiashara mmoja ambaye aliamua kufungua mgahawa wake. Wale wote ambao wameamua kuendesha shughuli zao na kukubali kuzungumza, wamesema kuwawamefanya hivyo ili kupata chakula cha leo. 'Maisha kwa kiwango cha siku' kama wanavyosema katika wa Kinshasa.

Mtu alionyesha suruali yake manjano na kupiga kelele, "ni kadi ya njano kwa Kabila Kabange". Karibu naye, watu walikusanya na kueleza: "Anapaswa kuzungumza na wapinzani wa kweli, kama mji ni uko katika hali hii, ni kutokana na hali ya sintofahamu inayojiri."

"Kabilaanapaswa kuondoke"

Katika kitongoji chenye watu wengi, vijana walionekana wakiwa na vipande vya karatasi ya manjano wameandamana, wakisema "Kabila anapaswa kuondoka." Mbali na hapo, polisi wamekua wakijaribu kuwatawanya waandamanaji kwa kurusha mabomu ya kutoa machozi. Baadhi ya vijana walikamatwa. Msemaji wa polisi amesema kwamba kumekuwa na matukio katika maeneo na baada ya waandamanaji kurusha mawe kwenye magari. Lakini hali kwa ujumla ilikua utulivu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.