Pata taarifa kuu
MAREKANI-SIASA

Wagombea kwenye nafasi ya Makamu wa rais marekani wakabiliana

Mgombea kwenye nafasi ya Makamu wa rais kutoka chama cha Democratic, Tim Kaine, na Mike Pence kutoka chama cha Republican walishiriki Jumanne hii usiku katika mjadala wa kisiasa utakaowakutanisha katika kampeni ya uchaguzi wa urais.

Tim Kaine (kushoto), mgombea mweza wa Hillary Clinton na Mike Pence,mgombea mweza wa Donald Trump,walikabiliana katika mjadala mkali Farmville, Virginia, Jumanne, Oktoba 4, 2016.
Tim Kaine (kushoto), mgombea mweza wa Hillary Clinton na Mike Pence,mgombea mweza wa Donald Trump,walikabiliana katika mjadala mkali Farmville, Virginia, Jumanne, Oktoba 4, 2016. REUTERS/Rick Wilking
Matangazo ya kibiashara

Mjadala huu inasemekana kuwa ulikua wa kiustaarabu ikilinganishwa na ule uliyofanyika kati ya Hillary Clinton na Donald Trump, lakini watazamaji hawajajua mengi kuhusu mtu atashikilia wadhifa huo.

Mjadala huu ulikua kati ya Gavana wa jimbo la Indiana kutoka chama cha Republican, Mike Pence, mwenye umri wa miaka 57, na Seneta wa jimbo la Virginia, Tim Kaine, mwenye umri wa miaka 58, wanasiasa wawili wenye uzoefu lakini hawana umaarufu.

Tim Kaine, ambaye alionekana mwenye hasira, alikua akimkatikiza mshindane wake alipokua akizungumza. Mike Pence, mpole, wakati mwingine alishindwa kutetea baadhi ya nafasi ya Donald Trump. Jambo ambalo Tim Kaine amepongeza. "Mara sita usiku wa leo, nimemwambia gavana Pence: " Sielewi jinsi gani unaweza kutetea nafasi ya mgombea wako faili baada ya nyingine. Na mara sita, alikataa mwenyewe kutetea mgombea mwenza wake."

Ni kweli kwamba kuhusu suala la uhamiaji kwa mfano, Mike Pence hakuweza kutetea pendekezo la Donald Trump la kuwafukuza mara moja wahamiaji haramu milioni 11wanaoishi nchini Marekani, endapo atabahatika kuwa rais wa Marekani.

"Wakati tutadhibiti mpaka, na si tu kujenga ukuta, wakati tutakua tumefanya yote hayo, tutarekebisha sheria za uhamiaji," amehakikisha mgombea mwenza wa Donald Trump

Mike Pence amesisitiza kwa kile anachoona kuwa ni kushindwa kwa sera ya Obama na Clinton nchini Iraq na Syria. Tim Kaine amekosoa sera ya Donald Trump ya 'kuunga mkono madikteta.' Putin ambaye alitajwa mara kadhaa katika mdahalo huo, alifanikia, kama hiyo ilikuwa ni nia yake, kuingilia kati katika kampeni za uchaguzi wa Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.