Pata taarifa kuu
MAREKANI-SIASA

Clinton na Trump kukabiliana katika mdahalo wa kwanza

Mdahalo wa kwanza kati ya wagombea wa urais nchini Marekani Hillary Clinton wa chama cha Democratic na Donald Trump wa chama Republican unafanyika Jumatatu hii, Septemba 26 usiku nchini Marekani.

Hillary Clinton (kushoto) na Donald Trump watakabiliana kwa muda wa dakika 90 mbele ya mamia ya watu walioalikwa kuhudhuria mdahalo huo.
Hillary Clinton (kushoto) na Donald Trump watakabiliana kwa muda wa dakika 90 mbele ya mamia ya watu walioalikwa kuhudhuria mdahalo huo. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mdahalo huu wa kwanza kati ya Bi. Clinton na Trump utaoneshwa kote duniani kupitia Televisheni na radio na unatarajiwa kuchukua muda wa dakika 90.

Wamarekani na watu wengine duniani watapata fursa ya kipekee kusikia kutoka kwa wagombea hao kuhusu maswala mbalimbali kama uchumi, usalama na sera zao kuhusu mambo ya nje.

Bi.Clinton mwenye umri wa miaka 68 anaangaziwa na wachambuzi wa mambo kama mtu anayefahamu maswala mengi kuhusu uongozi baada ya kuhudumu katika sekta ya utumizi wa umma kwa miaka 40, ikiwa ni pamoja na kuwa Waziri wa Mambo ya nje.

Donald Trump mwenye umri wa miaka 70, anayaefahamika kwa utajiri wake anafahamika kama mzungumzaji mzuri ambaye wachambuzi wanaona mara nyingi amekuwa hawezi kuelekezea kwa kina maswala muhimu yanayoikumba Marekani na dunia.

Uchaguzi nchini Marekani umepangwa kufanyika tarehe 8 mwezi Novemba, na kuelekea katika uchaguzi huo, kura ya maoni iliyofanywa na Gazeti la Washington Post inaonesha kuwa Clinton na Trump wanatoshana nguvu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.