Pata taarifa kuu
GABON-UCHAGUZI

Upinzani kuwasilisha madai yake mbele ya mahakama ya juu

Haijafahamika iwaapo upinzani nchini Gabon utawasilisha madai yake mbele ya Mahakama ya Katiba, baada ya kupinga kuchaguliwa tena kwa Rais Ali Bongo Ondimba. Sheria ya Gabon inabaini kwamba katika hali ya mzozo wa uchaguzi, wale ambao hawakuridhishwa na matokeo ya uchaguzi, wanatakiwa kuwasilisha madai yao mbele ya mahakama ya juu nchini.

Kiongozi mkuu wa upinzani Jean Ping, katika kampeni ya uchaguzi mjini Libreville, Agosti 29, 2016.
Kiongozi mkuu wa upinzani Jean Ping, katika kampeni ya uchaguzi mjini Libreville, Agosti 29, 2016. AFP/Marco Longari
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo upinzani haufikirii jambo hili, hasa kwa vile wengi wa wafuasi wake wanaamini kwamba Mahakama hiyo ni chombo kinachoendesha shughuli zake kwa maslahi ya Rais Ali Bongo. Upinzani unabaki na muda wa kuwasilisha madai yake hadi Alhamisi hii jioni.

Upinzani hauna imani na Mahakama ya Katiba, kwani unaamini kwamba chombo hiki kimekua kikishawishiwa na utawala. Kambi ya Jean Ping unashtumu kwanza muundo wa Mahakama ya Katiba, kwani majaji wake tisa wanachaguliwa na Rais wa Baraza la Seneti na rais wa nchi mwenyewe. Mkuu wa Mahakama anachaguliwa kutoka kwa majaji wa Mahakama hiyo walioteuliwa na Rais Bongo.

Swali ambalo watu wengi wamekua wakijiuliza, je upinzani utawasilisha madai yake mbele ya Mahakama ya Katiba? Kwa sasa, wapinzani wa Ali Bongo wanaomba hasa kuhesabiwa upya kwa kura mbele ya Tume ya Uchaguzi, chini ya uangaliazi wa wataalam. Jambo ambalo serikali inafutilia mbali, ikibaini kwamba sheria ya nchi haitaji utaraibu huo.

Licha ya hali ya utulivu kurejea katika maeneo mbalimbali nchini Gabon, mvutano wa kisiasa bado unaendelea, na hofu ya kutokea kwa machafuko zaidi imeendelea kutanda katika baadhi ya miji.

Makabiliano mjini Libreville kati ya wafuasi wa Ali Bongo Ondimba, aliyetangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais, na wale wa Jean Ping, Agosti 31, 2016.
Makabiliano mjini Libreville kati ya wafuasi wa Ali Bongo Ondimba, aliyetangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais, na wale wa Jean Ping, Agosti 31, 2016. AFP/Marco Longari

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.