Pata taarifa kuu
GABON-UCHAGUZI

EU: uchaguzi wa Gabon haukua wa wazi

Ujumbe wa uchunguzi wa Umoja wa Ulaya umesema kuwa uchaguzi wa urais wa siku ya Jumamosi nchini Gabon "haukua wa wazi".

Libreville, Agosti 27, zoezi la uhesabuji kura.
Libreville, Agosti 27, zoezi la uhesabuji kura. STEVE JORDAN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe wa Uchunguzi wa Umoja wa Ulaya umelaani "ukosefu wa orodha ya wapiga kura zilizowekwa nje ya vituo vya kupigia kura, kasoro katika udhibiti wa wino usiofutika, hitilafu katika uthibitisho wa kadi za kupigia kura na utaratibu wa utumiaji wa mihurikatia visanduku vya kura ".

Kiongozi wa ujumbe huo, Mariya Gabriel, amebainisha katika 17% ya vituo vya kupigia kura, "kesi ya kunyimwa haki ya kupiga kura kutokana na kukosekana kwa nyaraka halali za vitambulisho."

mariya Gabriel amesema kuwa taasisi za kusimamia zimeshindwa kutoa taarifa muhimu kwa pande husika kama vile orodha ya wapiga kura na orodha ya vituo vya kupiga kura.

Bi Gabriel amewapongeza wapiga kura wa nchini Gabon ambao walionyesha "nia yao ya kidemokrasia katika mchakato ambao usimamizi haukua wa wazi."

Bi Gabriel amewatolea wito viongozi kuendelea kutoa matokeo na kuyatangaza katika kila kituo cha kupigia kura ili kuhakikisha imani kwa wananchi.

"Baadhi ya makosa"

Kwa upande wake, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Gabonimesema ripoti ya waangalizi wa Umoja wa Ulaya ni sahihi, "licha ya baadhi ya makosa."

Katika taarifa yake, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Gabon imehakikisha kwamba "uchaguzi ulifanyika kwa amani na utulivu, bila ya ya vurugu, na utaratibu wa ya siri wa kura ilizingatiwa".

Matokeo rasmi ya uchaguzi yatatangaza Jumanne usiku wiki hii.

Kiongozi mkuu wa upinzani Jean Ping tayari amedai ushindi., huku rais anaye maliza muda wake Ali Bongo Ondimba akisema kuwa alishinda uchaguzi huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.