Pata taarifa kuu
GABON-UCHAGUZI

Wananchi wa Gabon wasubiri matokeo ya Uchaguzi mkuu

Nchini Gabon, matokeo ya uchaguzi wa urais yatatangaza Jumanne wiki hii saa 17 jioni, saa za nchini humo. Wengi wanakumbuka ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2009. Siku ya Jumapili, kila upande ulidai kuibuka mshindi. Jumapili jioni kulishuhudiwa hali ya utulivu katika mji wa Libreville.

Ali Bongo Ondimba (kushoto) na kiongozi mkuu wa upinzani  Jean Ping.
Ali Bongo Ondimba (kushoto) na kiongozi mkuu wa upinzani Jean Ping. REUTERS/Stringer/AFP/KenzoTribouillard/Montage RFI
Matangazo ya kibiashara

Rais anayetetea kiti chake nchini Gabon, Ali Bongo na mpinzani wake mkuu Jean Ping, kila mmoja amedai ushindi, kufuatia uchaguzi wa Rais uliofanyika nchini humo Jumamosi.

Katika baadhi ya maeneo ya mji huo, hasa katika kata ya ya Louis, kaskazini mwa mji huo, ambako watu wengi wamekua wakitembelea kwa kuja kupumzika, kulikua patupu. baa na migahawa ilikua imefungwa. Kulikua na utulivu usio wa kawaida, wakazi wa mji wa Libreville wamesema.

Mtazamo wa mji wa Libreville, mji mkuu wa Gabon.
Mtazamo wa mji wa Libreville, mji mkuu wa Gabon. photos-gratuites.org

Hali ya utulivu imeshuhudiwa pia katika mji wa pili wa Gabon wa Port-Gentil.

Maduja mengi Jumapili hii yalifungwa, huku katika mitaa mingi hapa kuweo na vikosi ya usalam au vya ulinzi. Hata hivyo wananchi wengi walikua na hofu ya kutokea kwa machafuko baada ya kila upande kudai ushindi.

Katika mkutano na vyombo vya habari Jumapili hii jioni mgembea katika uchaguzi huo kutoka kambi ya upinzani, Jean Ping alitangaza kuwa ameshinda uchaguzi, na anatazamia kuchukua hatamu ya uongozi wa nchi ziku chache zijazo.

"Nimeibuka mshindi katika uchaguzi wa urais na hivi karibuni najiandaa kuchukua hatamu ya uongozi wa nchi. Kwa sasa tuko katika kuuaga utawala wa Ali Bongo, " amesema Jean Ping.

Mwaka 2009, uchaguzi wa Ali Bongo ulipingwa vikali. Wakati huo mji wa Port-Gentil ulikumbwa na mapigano makali na uporaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.