Pata taarifa kuu
BURUNDI-UNSC

Chama cha CNDD-FDD chapinga azimio la UNSC

Katika tangazo lililotolewa Jumanne wiki hii, chama tawala nchini Burundi CNDD-FDD kimesema kuwa hakiwezi kutekeleza azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kutuma askari polisi 228 wa kimataifa kulinda usalama wa raia nchini Burundi hasa katika mji wa Bujumbura.

Chama tawala Burundi cha CNDD-FDD katika kampeni za uchaguzi wa urais 2010 Bujumbura.
Chama tawala Burundi cha CNDD-FDD katika kampeni za uchaguzi wa urais 2010 Bujumbura. AFP / Esdras Ndikumana
Matangazo ya kibiashara

"Bahati gani mbaya! Askari polisi 228 wa Umoja wa Mataifa dhidi ya Burundi, na Romeo Dallaire pamoja na Louise Albour kushirikiana na kikosi hiki," tangazo hilo limebaini.

Chama cha CNDD-FDD kimebaini kwamba tarehe 29 Julai 2016, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilitofautiana na kupitisha azimio 2,303 kwa kura 11 dhidi ya 4 ambazo hazikupinga au kukubali kutumwa kwa kikosi cha askari wa polisi 228. Kwa mujibu wa chama cha CNDD-FDD Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekwenda kinyume na maazimio yake lenyewe: 2248 la Novemba 12, 2015 na azimio 2279 la Aprili 1, 2016 kuhusu heshima kwa uhuru, uhuru wa taifa, mipaka ya taifa na umoja wa kitaifa wa Warundi.

Azimio hilo lilipitishwa bila kushauriana na serikali ya Burundi kama vile hakuna serikali ya Burundi iliyochaguliwa kwa misingi ya kidemokrasia, kimeendelea chama cha CNDD-FDD.

Chama hiki tawala nchini Burundi kimemshambulia kiongozi wa zamani wa kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Mataifa (UNAMIR), Romeo Dallaire, pamoja na Louise Arbour, Mwendesha mashitaka mkuu wa zamani katika Mahakama ya kimataifa kwa Rwanda (ICTR) yenye makao yake makuu mjini Arusha, nchini Tanzania.

Chama tawala nchini Burundi kimesema kinagaubaga kwamba kiongozi huyo wa zamani wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Rwanda (UNAMIR), aliwasaidia waasi wa zamani wa Rwanda wa RPF-INKOTANYI kufikia madaraka, baada ya kuwatimua wanajeshi wa zamani Rwanda katika utawala wa Juvenal Habyarimana.

Burundi imeendelea kukumbwa na hali ya sintofahamu, ambapo visa mbalimbali vya ukiukwaji wa haki za binadamu vimeendelea kuripotiwa. Machafuko nchini Burundi yamesababisha watu zaidi ya 500 kupoteza maisha na zaidi ya 280,000 kuyahama makazi yao.

Pascal Nyabenda, Spika wa Bunge la Burundi, akiwa pia kiongozi wa chama tawala cha CNDD-FDD.
Pascal Nyabenda, Spika wa Bunge la Burundi, akiwa pia kiongozi wa chama tawala cha CNDD-FDD. AFP PHOTO / LANDRY NSHIMIYE

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.