Pata taarifa kuu
NIGERIA-JAMII

Serikali ya Nigeria kuzungumza na chama cha wafanyakazi

Serikali ya Nigeria imepanga kuzungumza na viongozi wa chama cha wafanyikazi nchini humo ili kuzuia mgomo kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari. youtube
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya ajira nchini humo inasema inakutana na viongozi hao kujadili hatua ya serikali kuongeza bei ya Petroli kwa asilimia 67 wiki iliyopita.

Vyama vya wafanyikazi nchini humo vimetangaza kuanza mgomo wa wafanyikazi wote kuanzia kesho, kupinga kupanda kwa bei ya mafuta kutoka Naira 86 hadi 145.

Ikiwa mwafaka hautafikia kufikia kesho, shughuli za kawaida zitasitsihwa katika Ofisi za serikali, viwanja vya ndege, maduka makubwa na Benki.

Nigeria inategemea mapato yake kupitia asilimia 70 kutokana na biashara ya mafuta na ongezeko la bei ya mafuta limesababisha thamani ya Naira kushuka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.