Pata taarifa kuu
NIGERIA-AMNESTY

Amnesty yailishtumu jeshi la Nigeria kuwaua Waislamu 350 wa Kishia

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za Binadamu la Amnesty International limelishtumu jeshi la Nigeria kwa kuwauawa kwa kuwapiga risasi Waislamu 350 wa Kishia mwaka uliopita.

Katika wiki za hivi karibuni, Jeshi la Nigeria limeimarisha usalama kwenye ngome zake kaskazini mwa nchi, hasa katika jimbo la Maiduguri.
Katika wiki za hivi karibuni, Jeshi la Nigeria limeimarisha usalama kwenye ngome zake kaskazini mwa nchi, hasa katika jimbo la Maiduguri. AFP
Matangazo ya kibiashara

Shirika hilo limelaani madai ya jeshi kuwa kundi hilo kutoka vuguvugu la Islamic Movement of Nigeria waliokuwa wanaandamana, walikuwa na mpango wa kumuua mkuu wa majeshi nchini humo.

Jeshi, limekuwa likikisitiza kuwa Waislamu hao wa Kishia wamekuwa wakishirikiana na kundi la kigaidi la Boko Haram kuendelea kusababisha mauaji hasa Kaskazini mwa nchi hiyo.

Aidha, Msemaji wa Jeshi Brigedia Generali Rabe Abubakar amesema ripoti hiyo ya Amnesty sio sahihi na ni ya uonevu na wao kama jeshi hawakuwahi kushauriwa kabla ya kuchapishwa kwa ripoti hiyo.

Shirika hili limekuwa likiishtumu jeshi la Nigeria kwa kuendelea kuwahangasiha wafuasi wa kundi hili na kusisitiza kuwa uchunguzi wao umedhirihisha kuwa mauaji hayo yamekuwa yakitokea.

Mwezi Desemba mwaka jana, wafuasi wa kundi hili chini ya kiongozi waoIbrahim Zakzaky waliokuwa wanasiriki katika mkutano wao walipihswa risasi na wanajeshi baada ya kukataa msafara wa Mkuu wa majeshi kupita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.