Pata taarifa kuu
VENEZUELA-MVUTANO-SIASA

Venezuela yatangaza mabadiliko ya nyakati na kupanda kwa mishahara

Venezuela imebadili nyakati za nchi hiyo Jumapili hii kwa kuwa na kiwango cha kutosha kwa umeme, hatua iliyochukuliwa na rais kutoka chama cha Kisoshalisti Nicolas Maduro, ambaye anataka kuhamasisha wafuasi wake na kutuliza hasira ya wananchi kutokana na mgogoro kwa kuongeza mshahara wa chini.

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro aendelea kushikilia madaraka licha ya ya upinzani kuendesha harakati za kumng'oa kwenye wadhifa huo..
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro aendelea kushikilia madaraka licha ya ya upinzani kuendesha harakati za kumng'oa kwenye wadhifa huo.. REUTERS/Miraflores Palace
Matangazo ya kibiashara

Wakazi wa taifa hilo la Amerika ya Kusini walipotza usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili hii, nusu saa ya usingizi, kufuatia ta mabadiliko ya nyakati yaliyotangzwa na serikali: ilipofika saa 8:30 usiku wamejikuta wanatangaziwa kuwa ni saa 9:00 usiku. Kwa sasa muda wa kawaida nchini kote Venezuela umesogezwa mbele dakika thelathini.

Kabla ya mabadiliko hayo, mapema Jumamosi usiku, Rais Maduro, ambapo 68% ya watu wanaotaka aachiye ngazi kulingana na utafiti wa hivi karibuni, alitaka kuwatuliza nyoyo na kutangaza kwenye televisheni ongezeko la 30% kwenye mshahara wa chini.

Alikuwa na imani ya kuhamasisha wafuasi wake Jumapili hii katika siku ya wafanyakazi Mei 1, ambayo ingeliongozwa kwa maandamano muhimu mitaani.

Katika nchi hii inazozalisha mafuta, ambayo ni yenye uchumi unaokumbwa na kuporomoka kwa bei ya mafuta ghafi, serikali iliendelea kutangaza hatua katika wiki za hivi karibuni kwa kukabiliana na mgogoro, unaochochewa kwa sasa na uhaba umeme.

Venezuela inakabiliwa mara kwa mara na kukatika kwa umeme kutokana na matukio mbali mbali ya hali ya hewa kama El Niño, ambayo imesababisha ukame mbaya zaidi katika kipindi cha miaka 40, serikali imesema.

Baadhi ya hatua zilizotangazwa zinashangaza: watumishi katika sekta ya umma wanatakiwa kufanya kazi Jumatatu na Jumanne kwa wiki. Na karibu nchibi kote (isipokuwa Caracas), umeme utakatwa angalau masaa manne kwa siku.

Hali hiyo ilisababisha wiki hii iliyopita yenye maandamano na ghasia katika mji wa Maracaibo (kaskazini magharibi mwa nchi), mji wa pili kwa ukubwa wenye wakazi milioni 1.5.

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, mshahara wa chini tayari umeongezwa kwa 56%, baada ya kufikia 98% mwaka 2015.

Lakini hali hii inaonekana haitosha wakati ambapo nchi inakabiliwa na mfumuko wa bei mbaya zaidi duniani, 180.9% mwaka 2015, takwimu ambayo itafikia hadi 700% mwaka huu kwa mujibu wa Shirika la Fedha Duniani (IMF).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.