Pata taarifa kuu
VENEZUELA-MVUTANO-SIASA

Venezuela: Upinzani wataka kumng'oa Maduro mamlakani

Upinzani nchini Venezuela umekusanya Jumatano hii saini nchini kote kwa lengo la kuandaa ifikapo mwishoni mwa mwaka 2016 kura ya maoni dhidi ya rais kutoka chama cha Kisoshalisti, Nicolas Maduro.

Kiongozi wa upinzani  wa Venezuela na mkuu wa jimbo la Miranda, Henrique Capriles, akionyesha waraka unaolenga kutekelza kura ya maoni dhidi ya Nicolas Maduro, Caracas Aprili 26, 2016.
Kiongozi wa upinzani wa Venezuela na mkuu wa jimbo la Miranda, Henrique Capriles, akionyesha waraka unaolenga kutekelza kura ya maoni dhidi ya Nicolas Maduro, Caracas Aprili 26, 2016. AFP
Matangazo ya kibiashara

Nicolas Maduro anakabiliwa na shinikizo katika hali ya tata ya mgogoro wa kiuchumi na hasira ya raia.

Maelfu ya raia wa Venezuela wanasema kwa sasa wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha kutokana ukosefu wa ajira, wengine wakilazimishwa kutumika siku mbili kwa wiki katika sekta ya umma, huku umeme ukikatwa kwa muda wa masaa manne kwa siku kutokana na ukosefu wa nishati, na uchovu wa kusubiri mbele ya maduka makubwa yaliyo tupu. Raia hao wamekua wakijielekeza kwa siku ya jana katika maeneo mbalimbali yaliyotengwa ilikutia saini zao kwa kutokua na imani tena na Rais Nicolas Maduro.

"Nimekuja kutia saini ili kuuangusha utawala huu," Miriam Leal, mwenye umri wa miaka 54, kutoka mashariki mwa mji wa Caracas, ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP.

"Dawa zimekosekana, kazi na elimu pia hamna, mbali na hayo, kuna tatizo la umeme," Miriam Leal ameongeza, akieleza kwamba familia yake, "inateseka na kukatika kila mara kwa umeme".

"Hii ni kura ya maoni dhidi ya mgogoro," mmoja wa viongozi wa upinzani, Henrique Capriles, amesema, huku akitia saini kwenye waraka huo.

Mgombea aliyeshindwa katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2014, ana imani kwamba kambi yake itakusanya " kwa saa chache" saini 195,721 (sawa na 1% ya wapiga kura) zinazohitajika.

Hali ya mvutano

Kiwango hiki kinapaswa kufikiwa ndani ya siku 30, kisha kithibitishwe na Baraza la Kitaifa la Uchaguzi (CNE) ili kuingia katika hatua ya pili: kukusanya saini milioni nne ili kuandaa kura ya maoni, ambayo inaweza kufanyika mapema mwishoni mwa mwezi Novemba kwa mujibu wa Bw Capriles.

Itabdi kuzidisha idadi ya kura alizopata Nicolas Maduro mwaka 2014 (7,587,532) kwa kuweza kumng'oa mamlakani.

"Wapinzani hao wanapoteza muda wao. Wanachokifanya hakiendani na siasa au mapinduzi. Rais aliye madarakani ataendelea kuhudumu hadi mwaka 2018 utakapomalizika muhula wake," Rais Maduro amejibu Jumatano usiku, akimaanisha mwaka utakaofanyika uchaguzi ujao wa rais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.