Pata taarifa kuu
ICELAND-KASHAFA-UCHUMI

Iceland: Waziri Mkuu mpya aapishwa

Waziri Mkuu mpya wa Iceland, Sigurdur Ingi Johannsson, ameapishwa Alhamisi hii na rais, kuchukua nafasi ya Sigmundur David Gunnlaugsson, aliejiuzulu kufuatia shinikizo lililotokana na kuhusishwa kwake na kashfa ya ukwepaji kodi, iliyofichuliwa katika kampuni moja ya kisheria nchini Panama Mossack Fonseca.

Waziri Mkuu mpya wa Iceland Sigurdur Ingi Johannsson, mwenye umri wa kiaka 53.
Waziri Mkuu mpya wa Iceland Sigurdur Ingi Johannsson, mwenye umri wa kiaka 53. REUTERS/Sigtryggur Johannsson
Matangazo ya kibiashara

Iliaminika kuwa Gunnlaugsson anamiliki kampuni ya Wintris yeye na mke wake na kwamba hakuweka wazi umiliki huo baada ya kuingia katika Bunge la nchi hiyo.

Waziri huyo mkuu Iceland awali alikuwa akituhumiwa kuficha mamilioni ya dola na mali zinazomilikiwa na familia yake.

Sigmundur alisema kuwa alihamishia hisa za kampuni hiyo kwa mke wake na amepinga kuhusika na jambo lolote baya.

Kabla ya kiongozi huyo kujiuzulu, mamia ya watu walikuwa waliandamana mbele ya ofisi yake, walimtaka Waziri mkuu huyo aachiye ngazi.

Awali Jumanne Gunnlaugsson alipendekeza bunge la nchi hiyo livunjwe - pendekezo lilokataliwa na Rais Olafur Ragnar Grimsson. Gunnlaugsson alitoa pendekezo hilo baada ya upinzani kutaka kufanyike kura ya imani itakayopima kuwepo ama kutokuwepo kwa imani na serikali miongoni mwa wananchi.

Nyaraka zilizofichuliwa zilizopewa jina la "Panama Papers" zinaonyesha kwamba Waziri Mkuu huyo mwenye umri wa miaka 41 pamoja na mke wake wanamiliki kampuni kisiri nje ya nchi chini ya jina la Wintris Inc. Kampuni ambayo inadaiwa kuwa na kiasi cha dola milioni 4.2 katika benki tatu tofauti za Iceland zilizofilisika za Lansbanki, Glitnir na Kaupthing. Kampuni hiyo imedhihirishwa kuwa ilifunguliwa mwaka 2007 na Gunnlaugsson pamoja na mke mtarajiwa kwa wakati huwo Anna Sigurlaug Palsdottir.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.