Pata taarifa kuu
UFARANSA-KODI-UCHUMI

"Papers Panama": Mahakama ya Ufaransa yaanzisha uchunguzi wa awali

Uchunguzi wa awali kwa ajili ya "utajiri haramu kwa ukwepaji wa kodi" umeanzishwa na vMahakama ya Ufaransa Jumatatu hii, Aprili 4, kutokana na mafunuo katika vyombo vya habari kuhusu kesi ya "Panama Papers".

Rais wa chama cha FN, Marine Le Pen, katika mkutano na waandishi wa habari mjini Quebec,Machi 20, 2016.
Rais wa chama cha FN, Marine Le Pen, katika mkutano na waandishi wa habari mjini Quebec,Machi 20, 2016. AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Ofisi ya kitaifa ya mashitaka ya kifedha, mifumo ya ukwepaji wa kodi "huenda ikawahusu wakazi wa Ufaransa wanaotakiwa kulipa kodi."

Uchunguzi umekabidhiwa Taasisi kuu inayopambana dhidi ya uhalifu wa kifedha na kodi (OCLCIFF).

Wakati huo huo mmiliki wa kampuni ya Riwal na mtu wa karibu wa Marine Le Pen, Frédéric Chatillon, ni tu wa kwanza ambaye ameanza kuzungumzia Jumatatu hii kuhusu ufunuo wa kesi ya "Panama Papers" na kukinyooshea kidole cha lawama chama kikuu nchini Ufaransa cha FN.

"Ntakua na haki ya kuzungumza Jumanne hii kwa heshima gazeti la Le Monde kuhusu kesi hii," Chantillon ameandika kwenye ukurasa wa Facebook, kuhusu uwekezaji uliofanywa barani Asia, baada ya uchunguzi ulioweka wazi kashfa kubwa ya ukwepaji wa kodi inayowakabili viongozi wa kisiasa, wa michezo au mabilionea.

"Nilisikia kutoka kwa waandishi wa habari wawili walioweka wazi stakabadhi zinazothibitisha uhalali kamili wa shughuli hizo," Chantillon ameongeza.

Mkurugenzi wa gazeti Le Monde amebaini Jumatatu hii asubuhi kwamba ufunuo ujao katika kesi hii utakihusisha "chama kikuu cha kisiasa nchini Ufaransa."

Riwal ni kampuni ambayo inatoa huduma za mawasiliano kwa wagombea wa chama cha FN. Frédéric Chatillon, ambaye ni mmiliki wa kampuni hiyo amestakiwa kwa kosa la ufadhili haramu wa chama kama sehemu ya uchunguzi kuhusu uchaguzi wa rais na wa wabunge mwaka 2012.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.