Pata taarifa kuu
UFARANSA-KODI-LE PEN-UCHUMI

Tuhuma za udanganyifu wa kodi: msako waendeshwa nyumbani kwa Jean-Marie Le Pen

Wachunguzi wameendesha msako Jumatano wiki hii katika ofisi za Jean-Marie Le Pen katika mji wa Saint-Cloud (Hauts-de-Seine), katika kesi ihusuyo ukweli ukwepaji wa kodi na biashara haramu, vyanzo vilio karibu na faili hiyo na vyanzo vya mahakama vimeliambia shirika la habri la Ufaransa la AFP.

Kiongozi wa zamani wa chama cha National Front (FN), Jean-Marie Le Pen, Oktoba 16, 2015 katika mjini Marseille.
Kiongozi wa zamani wa chama cha National Front (FN), Jean-Marie Le Pen, Oktoba 16, 2015 katika mjini Marseille. AFP/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Uchunguzi unaomlenga mwanzilishi wa chama cha National Front (FN), ambaye uhusiano na chama chake umedorora, ulianzishwa mwezi Juni na Ofisi ya Mashtaka ya kitaifa ya Fedha (PNF). Uchunguzi huu unahusu masuala yanayoshukiwa kuwa ya udanganyifu wa kodi na kushindwa kutangaza mali yake, chanzo cha mahakama kimebaini.

Uchunguzi huu unahusiana na mfululizo wa ripoti ya kitengo cha kupambana na kujitajirisha kinyume cha sheria (Tracfin), kuhusu akaunti ya benki inayofichwa nje ya nchi, na Tume ya zamani inayoweka wazi Fedha katika maisha ya kisiasa, iliyobadilishwa tangu wakati huu Mamlaka kuu inayoweka wazi maisha ya umma (HATVP).

Mwishoni mwa mwezi Aprili, mtandao wa habari wa Mediapart ulibaini kutoa taarifa za Tracfin ukibaini kuwa ni akaunti iliyofunguliwa jijini Geneva, ambayo mmiliki wa akaunti hiyo ni msaidizi binafsi wa Jean-Marie Le Pen. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, akaunti hiyo inajaa kitita cha Euro milioni 2.2, ikiwa ni pamoja na milioni 1.7 zinazohifadhiwa katika mfumo wa dhahabu.

Jean-Marie Le Pen alikanusha kuhusika kwake katika mambo hayo ya kuwekeza mali yake nje ya nchi. " Ninakana jambo hilo. Sio kweli, kwa sababu Mediapart ikisema kitu , kichukuliwe kama ukweli wa injili ", Le Pen amesema.

Katika ripoti yake, Tracfin imetaja kuwepo kwa akaunti katika visiwa vya Virgin nchini Uingereza na kusimamiwa na Geneva kwa niaba ya msaidizi binafsi wa Jean-Marie Le Pen, kwa mujibu wa chanzo kilio karibu na faili hiyo kiliohojiwa na shirika la habari la Ufaransa AFP.

Kwa mujibu wa chanzo hiki, akaunti hiyo ilifungwa mwaka 2014 na fedha zilihamishiwa katika benki mjini Bahamas.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.