Pata taarifa kuu

AFCON 2023 : DR Congo yafuzu kwa nusu fainali baada ya kuishinda Guinea

Nairobi – Na Paul Nzioki

Wachezaji wa timu ya taifa ya DRC
Wachezaji wa timu ya taifa ya DRC AP - Themba Hadebe
Matangazo ya kibiashara

Timu ya taifa la DR Congo, iliifunga timu ya taifa la Guinea magoli 3-1 na kufuzu kwa hatua ya nusu fainali katika michunao ya kombe la mataifa ya Afrika AFCON, na kuifuata Nigeria iliyoishinda Angola.

Timu ya taifa la DR Congo, iliifunga timu ya taifa la Guinea na kufuzu kwa hatua ya nusu fainali katika michunao ya kombe la mataifa ya Afrika AFCON.

Mashabiki wa DRC wakati wa mechi kati ya nchi yao na Guinea
Mashabiki wa DRC wakati wa mechi kati ya nchi yao na Guinea © FMM

Mchezaji Arthur Masuaku, ambaye anacheza kama beki wa kushoto wa klabu ya Süper Lig ya Besiktas alifunga bao la tatu kuipa timu ya leopards ushindi wa 3-1.

Baada ya ushindi huo sasa, DRC watasubiri mshindi katika robo fainali inayomshirikisha mwenyeji wa michuano hii Côte d'Ivoire atakayecheza dhidi ya Mali.

Goli la pekee kwa Guinea lilifungwa na Mohamed Bayo, baada ya kuangushwa katika kijisanduku na nahodha wa leopards Chancel Mbemba.

Mbemba aliisaidia DRC kurudi mchezoni baada ya kufunga goli la kusawazisha huku mshambualiaji wa timu ya brendford ya England Yoane Wissa akifunga mkwaju wa penalty baada ya Masuaku kuangushwa katika kijisanduku.

Katika michuano ya mwaka huu, mechi ya jana ilikua ya kwanza kwa timu ya DRC kushinda mechi. Walimaliza wa pili katika kundi F baada ya kupata sare tatu, kundi likiongozwa na Morocco.Waliishinda Misri kupitia mikwaju ya penalti katika hatua ya 16 bora.

DRC imefuzu kwa hatua ya nne bora baada ya ushindi dhidi ya Guinea
DRC imefuzu kwa hatua ya nne bora baada ya ushindi dhidi ya Guinea © FMM

Guinea kwa upande wao walifuzu kama timu bora kati ya washindi wanne wa kufuzu kisha kuwaondoa Equatorial Guinea katika hatua ya 16 bora kwa mda wa kawaida.   

Katika historia ya mashindano ya AFCON Guinea nafasi yao bora ni kumaliza katika nafasi ya pili mwaka 1976 huku DRC wakiwa wameshinda taji hili mwaka 1968 na mwaka 1974.

DRC itakutana na mshindi kati ya Ivory Coast na Mali
DRC itakutana na mshindi kati ya Ivory Coast na Mali © FMM

Baada ya mechi kukamilika kocha wa Guinea Kaba Diawara alikosa maneno ya kusema kwa w&aandishi wa habari hata baada ya kusema alikua tayari kuwarudisha DRC nyumbani kabla ya mechi.

Leopards wanaongozwa na mfaransa Sebastien Desabre alionya wanaosema kua kuna matokeo ya kushangaza na kusema kua kwenye AFCON wanaoshinda na waliotia bidii.

Wachezaji wa timu ya taifa ya DRC wakati wa mechi dhidi ya Guinea
Wachezaji wa timu ya taifa ya DRC wakati wa mechi dhidi ya Guinea © FMM

Nigeria lilikua taifa la kwanza, kufuzu katika nusu fainali baada ya kuishinda Angola goli moja kwa bila goli lililofungwa na Ademola Lookman.

Nigeria watamsubiri mshindi katika robo fainali ya Cape Verde  dhidi ya Afrika Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.