Mechi za AFCON: DR Congo na Zambia zafungua kwa sare
NAIROBI – Yoane Wissa aliifungia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo bao la kusawazisha katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Zambia iliyomalizika kwa sare ya 1-1, baada ya kupokea pasi ya uhakika kutoka kwa Cedric Bakambu.
Imechapishwa:
Mechi hii ya kuwania taji la AFCON, ilichezwa Jumatano usiku kwenye mji wa Pwani wa San-Pedro.
Zambia ndio iliyokuwa ya kwanza kupata bao katika dakika za mapema za mchuano huo, kupitia mchezaji wake Kings Kangwa, aliyemchenga kipa wa DRC Lionel Mpasi.
Sare ya nchi hizo jirani, ilikuja baada ya Morocco, kuipa Tanzania kipigo cha mabao 3-0 katika mechi ya kwanza ya kundi la F.
Katika mchuano huo, Leopard ya DRC ilikuwa imepata penalti, lakini uamuzi huo ulibadilishwa na mwamuzi baada ya kubainika kuwa mchezaji Tandi Mwape hakuunawa mpira uliokuwa umepigwa na Arthur Masuaku.
Kocha wa Zambia Avram Grant, amesema licha ya matokeo hayo kutokuwa ya kuridhisha, mabingwa hao wa mwaka 2012, wanatarajia kufanya vema katika mechi mbili zinazosalia kati ya Morocco na Tanzania.
Chipolopolo sasa itachuana na Taifa Stars siku ya Ijumaa, wakati vijana wa kocha Sebastien Desabre wakichuana na Atlas Lions ya Morocco.
📹 𝗛𝗜𝗚𝗛𝗟𝗜𝗚𝗛𝗧𝗦: 🇲🇦 3-0 🇹🇿
— CAF (@CAF_Online) January 18, 2024
Strong start from the Atlas Lions as they score 3 past Zambia to win all 3 points. ✅#MARTAN | #TotalEnergiesAFCON2023 | @Football2Gether
Ratiba ya leo, Januari 18 2024
Equitorial Guinea V Guinea Bissau
Cote d’Ivoire V Nigeria
Misri V Ghana