Pata taarifa kuu

Saudi Arabia: Tuko tayari kuandaa michunao ya Kombe la Dunia la 2034

Shirikisho la kandanda la Saudia limesema liko tayari kuandaa michuano ya Kombe la Dunia la FIFA la 2034 wakati wa majira ya baridi au hata majira ya joto, kuhakikisha kwamba nchi hiyo inaweza kukabiliana na "uwezekano wote".

Kombe la Dunia la 2018 linaloshikiliwa na wachezaji wa timu ya Ufaransa, huko Moscow, Julai 15, 2018.
Kombe la Dunia la 2018 linaloshikiliwa na wachezaji wa timu ya Ufaransa, huko Moscow, Julai 15, 2018. AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Ufalme wa Ghuba, ambapo halijoto inaweza kupanda hadi nyuzi joto 50, illishindia nafasi ya kuandaa mashindano hayo chini ya mwaka mmoja baada ya michuano ya Kombe la Dunia kupigwa katika nchi jirani ya Qatar, ya kwanza kufanyika nje ya majira ya joto.

"Kuna teknolojia nyingi mpya zinazowezesha kupoza au kuongeza viyoyozi katika viwanja vya michezo, bila kusahau kwamba miji mingi nchini Saudi arabia ina hali ya kupendeza sana wakati wa kiangazi," mkuu wa shirikisho la kandanda nchini Saudia Yasser Al- Misehal aliliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumanne jioni.

"Tuko tayari kukabiliana na uwezekano wwoote," alihakikishia, kando ya hafla ya utoaji wa tuzo za Shirikisho la Soka la Asia (AFC) huko Doha.

Saudi Arabia, msafirishaji mkubwa zaidi wa ghafi duniani, ilituma maombi Oktoba 4, siku 27 kabla ya kufungwa kwa wito wa zabuni za Kombe la Dunia la 2030 na 2034.

Baada ya Kombe la Dunia la mwaka 2026 kuhusishwa na Marekani, Canada na Mexico, na lile la mwaka 2030 kwa Uhispania, Ureno na Morocco, ni nchi wanachama wa mashirikisho ya Asia na Oceania pekee ndizo zilizoalikwa kutuma ombi, kufuatia sera ya FIFA ya mzunguko wa mabara.

Kujiondoa kwa mgombea mwingine pekee katika kinyang'anyiro hicho, Australia siku ya Jumanne, kulifungua njia kwa Saudi Arabia kuchukua nafasi hiyo.

Uteuzi wake ulithibitishwa na rais wa shirikisho la soka duniani, Gianni Infantino, kwenye Instagram, ingawa faili rasmi ya maombi itawasilishwa na kupigiwa kura mwishoni mwa mwaka ujao.

Haki za binadamu

Ufalme huo wa kihafidhina, ambao ulifungua milango yake kwa watalii wa kigeni mnamo 2019, unatafuta kupunguza utegemezi wake wa mafuta kwa kuzingatia hasa michezo.

Chini ya uongozi wa mwana mfalme Mohammed bin Salman mwenye umri wa miaka 38, nchi hiyo imeongeza uwekezaji katika soka lakini pia Formula 1, gofu, mbio za farasi na ndondi.

Mamia ya mamilioni ya dola yametolewa mwaka huu na hazina yake ili kuwaajiri nyota wa kandanda, kama vile Cristiano Ronaldo, Neymar na Karim Benzema kwa vilabu vya Saudia.

Ufalme huo, hata hivyo, unakosolewa vikali kwa ukiukaji wake wa haki za binadamu, kwa mauaji ya mwandishi wa habari Jamal Khashoggi mnamo mwaka 2018, na vile vile kwa matumizi yake ya mara kwa mara ya hukumu ya kifo, sheria zake dhidi ya ushoga, usawa wa kijinsia na vikwazo vyake vya uhuru wa kujieleza.

Kukabidhiwa kwa Kombe la Dunia kwa Saudi Arabia "licha ya rekodi yake ya kutisha ya haki za binadamu (...) inaonyesha kwamba dhamira ya FIFA kwa haki za binadamu ni uongo mtupu", amelaani Minky Worden wa shirika la kimataifa la haki za Binadamu la Human Rights Watch.

Katika taarifa iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii Jumanne jioni, Shirikisho la Soka la Saudia lilisema "limejitolea kikamilifu kutimiza na kuvuka matakwa ya zabuni" likiangazia "shauku kubwa ya mchezo ndani ya taifa letu changa."

"Maombi ya pekee"

Kwa mujibu wa Yasser Al-Misehal, Saudi Arabia itawasilisha " zabuni ya pekee", kuwa nchi ya kwanza kuandaa Kombe la Dunia peke yake na timu 48.

Ingawa miji mingi ya Saudia hupata joto kali wakati wa kiangazi, baadhi hunufaika kutokana na hali ya hewa ya joto zaidi kama vile Abha, Taif au Al-Baha, ambapo Mashindano ya Kandanda ya Klabu za Kiarabu yalifanyika msimu wa joto uliopita.

Hakuna hata moja kati ya miji hii iliyo na miundombinu ya michezo inayolingana na tukio hilo, viwanja vikubwa zaidi vikiwa katika mji mkuu wa Riyadh, au katika mji wa pwani wa Jeddah.

Mbali na maswali yaliyoibuliwa na mchakato wa tuzo au haki za binadamu, Wasaudi wanafuraha kuandaa mashindano hayo maarufu zaidi duniani.

"Hizi ni habari nzuri na hazijitokezi popote pale," amesema Saud al-Oreifi, mkazi wa miaka 62 wa mji mkuu, akiangazia kuenea kwa matukio ya michezo katika ufalme huo. "Haya ni matokeo ya juhudi na mafanikio ya zamani."

Akiwa Riyadh, Mkuwait Thamer al-Choiebi pia amesema "anajivunia" kuona Saudi Arabia "inaheshimu sio tu Wasaudi, lakini ulimwengu wote wa Kiarabu."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.