Pata taarifa kuu
AFCON 2027

Je, Afrika Mashariki itapata fursa ya kuandaa michuano ya AFCON 2027 ?

Nairobi – Rais wa shirikisho la soka nchini Uganda, Moses Magogo ana imani Afrika Mashariki itashinda haki za kuandaa AFCON ya mwaka 2027.

Kongamano la biashara kuhusu michezo barani Afrika, lililofanyika jijini Nairobi, Septemba 15 2023
Kongamano la biashara kuhusu michezo barani Afrika, lililofanyika jijini Nairobi, Septemba 15 2023 © Jason Sagini
Matangazo ya kibiashara

Bado tuna muda, ili kupewa haki za kuandaa hawaangalii ulicho nacho bali mipango yako ni ipi

Moses Magogo alikuwa akizungumza kwenye kongamano la kibiashara la soka barani Afrika la mwaka 2023 lilioandaliwa jijini Nairobi nchini Kenya.

Uwanja wa Namboole nchini Uganda unaendelea kukarabatiwa
Uwanja wa Namboole nchini Uganda unaendelea kukarabatiwa © waziri wa michezo nchini Uganda

Moses anasisitiza kuwa kilichosukuma mataifa haya jirani kutuma ombi la pamoja ni kutokana na kuwa kwenye sheria za CAF, anayezingatiwa wa kwanza ni yule ambaye hajawahi kuandaa mashindano.

Licha ya hayo, Afrika Mashariki tayari ina viwanja kadhaa – Nyayo, Eldoret, Moi Kasarani, Ulinzi Sports Complex, Benjamin Mkapa ambayo itaandaa mechi ya ufunguzi ya ligi ya supa Afrika, kwa hivyo hakuna haja ya kujenga viwanja vipya kama ilivyo na wapinzani wao ila tu kufanyia viwanja ukarabati. 

Mwanachama wa kamati ya FUFA, Rogers Byamukama, anasema serikali ya Tanzania imeanza mikakati ya ujenzi wa uwanja wa mashabiki elfu tisini mjini Arusha.

Ukarabati wa uwanja wa Abed Karume unaelekea kukamilika. Nchini Uganda, uwanja wa Namboole na Nakivubo utakamilika mwezi Novemba na Disemba mtawalia. 

Tunahitaji tu uwanja mmoja wa mashabiki elfu arubaini katika kila nchi na viwanja vingine vya mashabiki elfu kumi na tano 

Uwanja wa Kimataifa wa Moi Kasarani jijini Naiorobi nchini Kenya
Uwanja wa Kimataifa wa Moi Kasarani jijini Naiorobi nchini Kenya pbs.twimg.com/medi

Afrika Mashariki ina idadi ya watu zaidi ya milioni mia mbili ambayo taifa la Nigeria pekee ndilo linazidi idadi hiyo.

Kutokana na kuwa na mataifa matano kutoka afrika mashariki katika mataifa kumi na tano bora kiuchumi barani Afrika, idadi hii ya watu kama anavyosema rais Magogo utasaidia kuipa CAF mapato zaidi kuliko wapinzani wao kwenye kuandaa – Misri na Algeria.  

Ukanda huu pia ni eneo sahihi kwa utalii wa wageni. Kati ya milima mirefu zaidi mitano ulimwenguni, tatu zinapatikana afrika mashariki – mlima Ruwenzori, mlima Kenya na Kilimanjaro kando na kuwa na mbuga za wanyama zenye aina tano kubwa za wanyama. 

Rogers Byamukama anasisitizia kuboreka kwa usafiri kutokana na reli ya SGR kuunganisha Uganda na Kenya, safari za ndege huchukua saa moja kusafiri kati ya miji mikuu mitatu na barabara za kisasa.  

Pia tuna hoteli za kisasa ambazo ni bora kuliko wenzetu. Nini kingine kitazuia Afrika Mashariki kuandaa kama si sasa?

Rais Moses Magogo anasema pia kuandaa kombe hili kutanufaisha kila mtu kwa mataifa haya kuanzia kwa wafanyabiashara, mashabiki na ligi za ukanda.  

Tunafaa tuwe tayari kufikia Januari mwaka 2026 na tuko mwaka 2023, naamini tutaileta Afrika nzima ndani ya Afrika Mashariki.

Mshindi wa kuandaa makala ya mwaka 2025 pia atatangazwa tarehe 27 Septemba. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.