Pata taarifa kuu

Bayern yathibitisha uhamisho wa Mane kuenda Saudi

Nairobi – Bayern Munich imetangaza kwamba mshambuliaji wa Senegal, Sadio Mane amekuwa kwenye mazungumzo nao kuhusu umahimisho wake ripoti zikionyesha kuwa anatarajiwa kwenda Al Nassr ya Saudi.

 Sadio Mané, anatarajiwa kuhamia katika ligi ya Saudi Arabia
Sadio Mané, anatarajiwa kuhamia katika ligi ya Saudi Arabia REUTERS - MATTHIAS RIETSCHEL
Matangazo ya kibiashara

Mabingwa hao wa Ujerumani walimwacha Mane nje ya mechi ya kirafiki mjini Tokyo, wakiandika kwenye Twitter, "Sadio Mane yuko kwenye mazungumzo ya kandarasi mpya na klabu nyingine ikiwa ndio sababu hayumo kwenye kikosi."

Nyota huyo wa zamani wa Liverpool mwenye umri wa miaka 31 anatazamiwa kuwa mchezaji wa hivi punde zaidi wa hadhi ya juu kujiunga na ligi ya Saudia yenye pesa nyingi.

Jarida la Bild na Kicker limeripoti kuwa Mane amebakisha kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na Al Nassr kama hatua ya mwisho ya kujiunga na klabu hio.

Sadio Mané alijunga na Bayern akitokea Liverpool
Sadio Mané alijunga na Bayern akitokea Liverpool REUTERS - HEIKO BECKER

Raia huyo wa Senegal, atakuwa mchezaji mwingine mkubwa kusajiliwa na klabu hiyo baada ya kumnasa Cristiano Ronaldo, mshindi mara tano wa tuzo ya Ballon d'Or mwaka uliopita.

Mane tayari ameshinda kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya na taji la Ligi nchini Engaldn katika misimu sita akiwa na Liverpool na alikuwa sehemu muhimu ya safu ya ushambualiaji ya Jurgen Klopp akiwa na Mohamed Salah na Roberto Firmino.

Wakati Liverpool ikishinda taji lao la kwanza la ligi ya Uingereza kwa miaka 30 katika msimu uliotatizika wa 2019-2020, Mane alifunga mabao 18.

Mane atajiunga na Cristiano Ronaldo katika ligi hiyo ya Saudi Arabia.
Mane atajiunga na Cristiano Ronaldo katika ligi hiyo ya Saudi Arabia. AFP - FAYEZ NURELDINE

Katika majira ya joto ya 2022, aliposhinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika wa mwaka, Mane aliamua kwamba anataka changamoto mpya, uvumi ambao haujathibitishwa ulisema kuwa amechoka kushiriki chini ya utukufu wa Salah wa Misri huko Anfield.

Baadae alijiunga na Bayern Munich ya Ujerumani wakiahidi kumfanya awe kitovu cha safu ya ushambuliaji ambayo ilikuwa imepoteza huduma za Robert Lewandowski alipojiunga na Barcelona.

Mwanzoni mwa mwaka 2023 Mane alihusika katika ugomvi na Leroy Sane kufuatia klabu yao kushindwa katika ligi ya mabingwa na Manchester City.

Bayern ilimpiga Mane faini ya takriban euro 350,000 ($385,000) na kumpa adhabu ya kutocheza mechi moja kwa upande wake katika tukio hilo.

Sadio Mané anakuwa mchezaji wa hivi punde kujiunga na ligi ya nchini Saudi Arabia
Sadio Mané anakuwa mchezaji wa hivi punde kujiunga na ligi ya nchini Saudi Arabia REUTERS - PHIL NOBLE

Al Nassr atajiunga na Ronaldo, kiungo wa kati wa Croatia Marcelo Brozovic, beki wa pembeni wa Brazil Alex Telles na kiungo wa Ivory Coast Seko Fofana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.