Pata taarifa kuu

Kombe la dunia: Marekani imetoka sare ya bao 1 kwa 1 na Uholanzi

Nairobi – Katika michuano ya kombe la dunia kwa wanawake katika mchezo wa soka, inayoendelea nchini New Zealand na Australia.

Marekani na Netherlands zimetoka sare ya bao moja kwa moja
Marekani na Netherlands zimetoka sare ya bao moja kwa moja REUTERS - AMANDA PEROBELLI
Matangazo ya kibiashara

Marekani imetoka sare ya bao 1 kwa 1 na Uholanzi, katika mechi ya kundi E iliyomilikiwa saa chache zilizopita.

Baadaye leo, katika mji wa Dunedin, nchini New Zealand, Ureno itachuana na Vietnam, katika mechi ya kundi E huku, Australia nayo itamenyana na Nigeria katika mechi ya kundi B.

Katika mechi ya kwanza, Nigeria haikufungana na Canada ambayo jana katika mechi yake ya pili, iliishinda Jamhuri ya Ireland mabao 2 kwa 1 .

Marekani na Netherlands zimetoshana nguvu baada ya kutoka sare ya bao moja kwa moja
Marekani na Netherlands zimetoshana nguvu baada ya kutoka sare ya bao moja kwa moja REUTERS - AMANDA PEROBELLI

Wawakilishi wengine wa Afrika, Zambia jana walicharazwa mabao 5 kwa 0 na Hispania katika mechi ya kundi C, mechi ya kwanza Zambia pia ilifungwa mabao 5 kwa 0 na Japan.

Afrika Kusini na Morocco pia ni wawakilishi wengine wa Afrika na hawajapata ushindi wowote mpaka sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.