Pata taarifa kuu

Ogier apata ushindi siku ya pili ya mashindano ya Safari Rally

Na: Jason Sagini

Mashindano ya kimataifa ya kukimbiza magari nchini Kenya
Mashindano ya kimataifa ya kukimbiza magari nchini Kenya © Safari Rally Kenya
Matangazo ya kibiashara

Mfaransa Sebastien Ogier, amepata matokeo mazuri katika hatua mbalimbali ya mashindano ya Kimataifa ya kukimbiza magari, Safari Rally, yanayoendelea Naivasha nchini Kenya.

Bingwa huyo mara nane wa dunia, licha ya kutatizwa na wanyamapori hasa punda milia, alifanikiwa kupata ushindi katika hatua tatu za mwisho, mbele ya wapinzani wake Finn Rovanpera na Welshman Elfyn.

Mashindano ya Safari Rally, Naivasha Juni 23 2023
Mashindano ya Safari Rally, Naivasha Juni 23 2023 © Safari Rally Kenya

Madereva bado wana hatua sita, siku ya Jumamosi na Jumapili ili kumpata mshindi wa mashindano hayo, huku Rovanpera akipambana kutetea ubingwa wake.

Ogier, alishinda taji la mwaka 2021 wakati mashindano ya Kenya, yaliporejeshwa kwenye mashindano ya dunia.

Mashindano hayo yalianza siku ya Ijumaa jijini Nairobi, ambapo raia wa Estonia Ott Tänak alianza harakati yake ya kushinda ubingwa wake wa kwanza barani Afrika, baada ya kushinda mkondo wa kwanza wa ufunguzi wa Kasarani. 

Bingwa huyo wa makala ya mwaka 2019 alimshinda dereva wa Ufaransa Sebastien Ogier kwa sekundi 0.1 baada ya kukamilisha kilomita 4.84 katika uwanja wa kimataifa wa michezo wa Moi Kasarani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.