Philippe Diallo amechaguliwa kuwa rais mpya wa Shirikisho la Soka la Ufaransa
NAIROBI – Diallo ambaye amekuwa akishikilia majukumu ya uongozi wa muda katika shirikisho hilo baada ya kujiuzulu kwa kiongozi wa muda mrefu Noel Le Graet, amechukua nafasi hiyo baada ya kushinda kwa zaidi ya asilimia 90 ya kura za wanachama 200 katika mkutano mkuu wa FFF mjini Paris.
Imechapishwa:
Philippe mwenye umri wa miaka 59 anatarajiwa kuongoza shirikisho hilo hadi miwshoni mwa mwaka wa 2024.
Akizungumza baada ya uteuzi wake Diallo ameeleza kuwa hatua ya kuchaguliwa kwake ni heshima kubwa na kuwashukuru waliompigia kura.
Aidha amesema kuwa ni jukumu kubwa ambalo amepewa baadaya kile amesema kwamba wamevumilia katika nyakati ngumu katika miezi michache iliyopita.
Diallo alichukua nafasi ya kaimu rais mwezi Januari wakati Le Graet alipojiondoa kwa mara ya kwanza na kisha kulazimika kujiuzulu kufuatia shutuma za unyanyasaji wa kijinsia na kumaliza zaidi ya muongo mmoja wa uongozi wake katika shirikisho.
Hatua ya kujiuzulu kwa Le Graet kulikuja siku chache baada ya kuchapishwa kwa ripoti mbaya ya usimamizi katika shirikisho la FFF yenye makao yake makuu mjini Paris, ambayo ilikuwa imeagizwa na wizara ya michezo.
Wakati huo huo mchezo wa wanawake nchini Ufaransa ulikuwa unakabiliwa na changamoto baada ya Corinne Diacre kutimuliwa kama kocha wa timu ya taifa wakati nafasi yake ilipodhoofika kufuatia uasi wa wachezaji wakuu.