Faith Kipyegon wa Kenya ameandikisha rekodi mpya katika mbio za mita 1500
NAIROBI – Raia wa Kenya Faith Kipyegon aliweka rekodi mpya ya dunia ya mita 1500 katika mbio za Diamond League mjini Florence Italia siku ya Ijumaa, huku Muingereza Laura Muir akimaliza katika nafasi ya pili.
Imechapishwa:
Kipyegon aliweka rekodi mpya baada ya kukimbia kwa dakika 3 sekunde 49.11, na kuvunja rekodi ya awali ya dakika 3:50 kwa mara ya kwanza, huku Muir akikimbia kwa muda bora wa msimu wa 3:57.09.
Genzebe Dibaba wa Ethiopia aliweka rekodi ya awali ya saa 3:50.07 mwaka 2015.
Ciara Mageean wa Ireland pia alikimbia wakati bora zaidi wa msimu alipomaliza wa nne kwa 4:00.95.
Viongozi mbalimbali kutoka nchini Kenya akiwemo rais William Ruto na kinara wa upinzani Raila Odinga wamempongeza mwanariadha huyo baada ya kuweka rekodi mpya ya mbio hizo.
Hardwork, determination and consistency has been crowned this evening. Congratulations Faith Kipyegon for shattering the 1500m World Record in Florence, Italy and writing your name in the history of athletics. pic.twitter.com/zKhw9z4PVJ
— William Samoei Ruto, PhD (@WilliamsRuto) June 2, 2023
Kipyegon ameshinda dhahabu ya dunia na Olimpiki mara mbili lakini hii ni mara yake ya kwanza kuvunja rekodi ya dunia.
Sasa anashikilia mara ya kwanza na ya tatu kwa kasi zaidi katika historia, akitumia ubora wake wa awali wa 3:50.37 Agosti iliyopita.