Pata taarifa kuu

Kenya, Uganda na Tanzania kutangaza ombi la kuandaa AFCON 2027

NAIROBI – Kenya, Tanzania na Uganda zinataka kuandaa kwa pamoja michuano ya kombe la soka kwa mataifa ya Afrika AFCON mwaka 2027. 

Mataifa ya Kenya, Uganda na Tanzania yanataka kuwa mwenyeji wa AFCON 2027
Mataifa ya Kenya, Uganda na Tanzania yanataka kuwa mwenyeji wa AFCON 2027 © State House Kenya
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatatu, rais wa Kenya William Ruto alipokea ujumbe huo kutoka kwa Waziri wa Michezo Ababu Namwamba na kumpa idhini ya kuendelea na mchakato huo. 

"Tumeungana na ndugu zetu wa Uganda na Tanzania katika kuweka ombi la pamoja kwa Shirikisho la Soka barani Afrika CAF ili kupata fursa ya kuandaa AFCON 2027. Hakuna nchi yoyote iliyopata fursa ya kuandaa michuano hiyo ya kifahari kufikia sasa," Ruto alisema. 

"Tunatambua kwamba talanta zipo katika tasnia ya michezo na ubunifu nchini Kenya na zinahitaji kuunganishwa. Tunanuia kikamilifu na  kukuza uchumi wa michezo na ubunifu," aliongeza. 

Matamshi ya rais yanakuja siku moja baada ya kutazama mechi ya Mashemeji derby pamoja na kiongozi wa upinzani Raila Odinga katika uwanja wa Nyayo, ambapo AFC Leopards walipata ushindi. 

Ruto pia alikuwepo Jumamosi katika onyesho la Kip Keino classic lililoandaliwa katika uwanja wa kimataifa wa Moi, Kasarani 

Kinara upinzani nchini Kenya Raila Odinga na rais William Ruto walihudhuria mashindano ya riadhaa ya Kip Keino Classic jijini Nairobi
Kinara upinzani nchini Kenya Raila Odinga na rais William Ruto walihudhuria mashindano ya riadhaa ya Kip Keino Classic jijini Nairobi © State House Kenya

"Sekta hii ni chemchemi kubwa ya fursa za kuajiri mamilioni ya vijana, kuongeza mapato, kukuza pesa kwa kitaifa na kuiweka Kenya katika nafasi inayostahili kama nguvu kuu ya riadha na michezo," Ruto alisema. 

Kenya imefuzu mara tano kwa AFCON (1972, 1988, 1990, 1992 na 2019). 

Kenya, Uganda na Tanzania zinataka kuwa mwenyeji wa AFCON 2027
Kenya, Uganda na Tanzania zinataka kuwa mwenyeji wa AFCON 2027 © State House Kenya

Tanzania ilicheza mara mbili katika mashindano hayo (1980 na 2019) huku Uganda Cranes ikishiriki mara saba

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.