Barcelona ndio mabingwa wa La Liga
NAIROBI – Barcelona inasherekea ushindi wao wa kwanza wa Ligue ya Uhispania tangu kuondoka kwa Lionel Messi katika klabu hiyo miaka miwili iliyopita wakati timu hiyo iliôkuwa inakabiliwa na changamoto za kifedha.
Imechapishwa:
Kalbu hiyo ya Uhispania ilipata ushindi wa magoli manne kwa mawili dhidi ya Espanyol siku ya Jumapili katika mechi ambayo ilishuhudia mashabiki wa Espanyol kuingia katikati ya uwanja baada ya mechi, hali iliyowalazimu wachezaji wa Barcelona kuondoka.
Robert Lewandowski alifunga mabao mawili, magoli yalioisadia klabu hiyo kupata taji lao la kwanza tangu mwaka wa 2019. Hatua hi ikija licha ya mechi nne kusalia kabla ya kumalizika kwa msimu.
That title-winning feeling 🏆 pic.twitter.com/RxhyyDaM7w
— FC Barcelona (@FCBarcelona) May 15, 2023
Mara ya mwisho kwa Barcelona kusherehekea ushindi wa ligi bila ya kuwepo kwa Messi katika kikosi chake ilikuwa mwaka wa 1998-99. Messi alijiunga na kikosi cha kwanza cha Barcelona mwaka wa 2004-05 na kisha kushinda taji la ligi msimu huo.
Sherehe za wachezaji wa klabu hiyo uwanjani baada ya mechi zilikatizwa baada ya tukio la mashabiki wa Espanyol kuingia uwanjani na kuaanza kuimba na kusherehekea na wachezaji hao.
🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾
— FC Barcelona (@FCBarcelona) May 14, 2023
🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾
🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾
🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾
🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾
🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾
🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾
🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾
🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾
🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍾 pic.twitter.com/CJwVQCs0s6
Maofisa wa usalama walilazimika kuingilia tukio hilo kwa haraka kuwazuai mashabiki Zaidi kuingia. Alejandro Balde na Jules Koundé pia nao waliifungia Barcelona, ambao kwa sasa wanamataji 27.
Ushindi huo dhidi ya mahisimu Espanyol uliwapa Barcelona alama 85 baada ya mechi 34, wakiwa pia na alama 14 zaidi ya Real Madrid, ambao waliwashinda Getafe kwa bao moja bila ya jibu siku ya Jumamosi.