Pata taarifa kuu

Uganda: FUFA yawafungia waamuzi na wachezaji kwa visa vya upangaji matokeo

NAIROBI – Shirikisho la soka nchini Uganda, FUFA limetoa adhabu ya kufungiwa kwa muda, kwa wachezaji sita na waaamuzi wawili kutokana na tuhuma za upangaji matokeo katika mechi za Soka. 

Baadhi ya waamuzi na wachezaji nchini Uganda wapewa adhabu kwa tuhuma za upangaji wa matokeo ya mechi
Baadhi ya waamuzi na wachezaji nchini Uganda wapewa adhabu kwa tuhuma za upangaji wa matokeo ya mechi © Getty Images/iStock/Artisteer
Matangazo ya kibiashara

Washirika waliopigwa marufuku ni pamoja na waamuzi Opio Deogracious na Nkurunziza George. 

Wachezaji ni Waiswa Andrew, Kakooza Yaya Mahad wanaoichezea Gaddafi FC, mchezaji wa Kitara FC Lwesibawa Godfrey, Maganda Saleh ambaye ni mlinda lango wa timu ya Calvary FC. 

Pia mlinda lango wa timu ya Northern Gateway FC Oringa Franco na Mwima Abdallah anayeichezea timu ya chuo kikuu cha Ndejje wanakamilisha orodha ya waliofungiwa. 

Uamuzi huo umetolewa baada ya kamati ya uchunguzi katika kamati ya maadili na nidhamu ya FUFA kufanya kikao na kusema uamuzi wao unazingatia Ibara ya 73 ya Kanuni za Maadili na Nidhamu za FUFA. 

Wanasoka hao wamesimamishwa kwa muda kujihusisha na shughuli zozote za soka (utawala, michezo au nyingine yoyote) katika ngazi ya taifa kwa muda wa siku 90. Kusimamishwa kwa muda kunaanza kutumika mara moja. 

Mahakama ilichukua maamuzi kufuatia kukiri kwa watu binafsi na data inayopatikana kutoka kwa ripoti za uadilifu katika mechi. 

Kwa mujibu wa ibara ya 72 ya kanuni za maadili na nidhamu za FUFA, kamati ya upelelezi ilibaini kuwa kuna kesi ya msingi na taratibu za upelelezi zimefunguliwa dhidi ya watu wanane waliosimamishwa kwa muda kwa uwezekano wa ukiukaji wa Ibara ya 41 (Kuchezea mechi za soka), kifungu cha 42.(kushindwa kuripoti), kifungu cha 38 (Kamari), kifungu cha 14 (Kanuni za Jumla za Maadili).

Haya ni kwa mujibu wa katiba inayoongoza shirikisho la Soka nchini humo. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.