Pata taarifa kuu

Kombe la Dunia-2022: Qatar kuidhinisha uuzaji wa bia wakati wa mechi, kwa masharti

Uuzaji wa bia utaruhusiwa chini ya ya baadhi ya masharti kwa watu watakaohudhuria mechi za Kombe la Dunia la FIFA nchini Qatar, chanzo kinachofahamu suala hilo kimesema Jumamosi. 

Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Qatar Airways Akbar al-Baker akiwa katika mkutano na Namba mbili wa kamati ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia-2022 Hassan al-Thawadi, Desemba 12, 2016 huko Doha.
Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Qatar Airways Akbar al-Baker akiwa katika mkutano na Namba mbili wa kamati ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia-2022 Hassan al-Thawadi, Desemba 12, 2016 huko Doha. AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Mashabiki walio na tikiti wataweza kununua bia wakati wa mechi, katika muda wa saa tatu kabla ya mechi na saa moja baada ya filimbi ya mwisho.

Qatar itawaruhusu watu wanaohudhuria mechi za kandanda za Kombe la Dunia, zitakazoandaliwa mwishoni mwa mwaka huu nchini humo, kununua bia chini ya baadhi ya masharti, kulingana na chanzo kinachofahamu suala hilo.

Ni mara ya kwanza kwa michuao ya Kombe la Dunia kufanyika katika nchi ya Kiislamu ambapo uuzaji wa pombe umedhibitiwa vikali, jambo ambalo linaleta changamoto kubwa kwa waandaji, wakati hafla hiyo ikidhaminiwa na kampuni kubwa ya bia.

"Itawezekana kununua bia mara tu milango itafunguliwa, saa tatu kabla ya kuanza. Yeyote anayetaka kununua bia ataweza kufanya hivyo. (Mashabiki) pia wataweza kununua wakati wa saa moja baada ya kupulizwa kipenga cha mwisho,” kimeeleza chanzo hicho.

Kombe la Dunia ladhaminiwa na Budweiser

Budweiser, mmoja wa wafadhili wakubwa wa Kombe la Dunia, ataruhusiwa kuuza bia katika sehemu ya eneo kuu la mashabiki, lililoko katikati mwa Doha, kuanzia saa 6.30 jioni hadi saa saba usiku kila siku wakati wa mashindano, chanzo hicho kimesema.

Katika michuano ya Kombe la Dunia iliyopita, bia ilitolewa siku nzima katika "maeneo ya mashabiki".

Bei ambayo bia hizo zitauzwa bado inazingatiwa, chanzo kimesema.

Ingawa pombe haijapigwa marufuku kabisa nchini Qatar, unywaji wake katika maeneo ya umma umepigwa marufuku. Wasafiri hawawezi kuingia nchini ikiwa wamebeba pombe, hata kama wameinunua kutoka kwa maduka ya "duty free" ya uwanja wa ndege.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.