Pata taarifa kuu
CAF-SOKA-KLABU

Taji la Shirikisho : TP Mazembe yafuzu robo fainali, Simba yakwama

Klabu ya soka ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imefuzu katika hatua ya robo fainali, kuwania taji la Shirikisho barani Afrika, baada ya kulamisha sare ya mabao 2-2 dhidi ya AS Otoho ya nchi jirani ya Congo Brazaville.

Mshambuliaji wa Tout Puissant Mazembe  Christian Koffi f akimenyana na Soufiane Rahimi, wa Raja Casablanca   Februari 28 2020.
Mshambuliaji wa Tout Puissant Mazembe Christian Koffi f akimenyana na Soufiane Rahimi, wa Raja Casablanca Februari 28 2020. STR/AFP
Matangazo ya kibiashara

Mazembe ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia Beni Kinzumbi katika dakika ya 35, lakini Wilfid Nkaya akaisawazishia AS Otoho katika dakika ya 66 kipindi cha pili.

Bao la pili la TP Mazembe lilifungwa na Christian Koffi katika dakika ya 83 lilionekana kuipata ushindi klabu hiyo  lakini Jaures Ngombe alididimiza ushindi wa wageni wao kwa kusaisawazishia AS Otoo katika dakika ya 87.

Kuelekea mechi ya mwisho, dhidi ya Al Masry katika uwanja wao wa nyumbani Aprili 3 mjini Lubumbashi, Mazembe ni wa pili katika kundi C kwa alama nane, huku Al Masry ikiongoza kwa alama 10.

Nayo Simba Sports Club ya Tanzania, ilikuwa dhaifu mbele ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast baada ya kufungwa mabao 3-0.

ASEC Mimosas ilipata manbao mawili katika kipindi cha kwanza kupitia Aubin Kramo dakika ya 16, Stephane Ki akafunga la pili katika dakika 25 huku Karim Konate akifunga la tatu katika dakika ya 57.

Matokeo hayo yanaicha Simba na alama saba, huku mechi yake ya mwisho ikiwa dhidi ya  Union Sportive de la Gendarmerie Nationale ya Niger, jijini Dar es salaam Aprili tatu.

Matokeo kamili mechi zilizochezwa Machi, 20 2022.

  • Zanako 1 - 0 CS Sfaxien
  • Al-Masry 2 - 0 Cotonsport
  • Al-Ittihad 3 - 2 Royal Leopards
  • Otoho d'Oyo 2 - 2 TP Mazembe
  • USGN 2 - 2 RSB Berkane
  • ASEC Mimosas 3 - 0 Simba
  • Al Ahli Tripoli 1 - 0 Pyramids
  • Saoura 0 - 2 Orlando Pirates
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.