Pata taarifa kuu
TENNIS-FRENCH OPEN 2021

Tennis: Djokovic bingwa wa taji la French Open

Novak Djokovic alitoka nyuma kwa seti mbili na kumshinda Stefanos Tsitsipas raia wa Ugiriki kwa seti za 6-7(6) 2-6 6-3 6-2 6-4 na kushinda taji la mchezo wa Tennis la French Open kwa mara ya pili.

 Novak Djokovic bingwa wa taji la French Open kwa upande wa wanaume. 13 Juni 2021
Novak Djokovic bingwa wa taji la French Open kwa upande wa wanaume. 13 Juni 2021 Anne-Christine POUJOULAT AFP
Matangazo ya kibiashara

Fainali hiyo iliyofanyika siku ya Jumapili, Juni 13 2021 jijini Paris, sasa imemwongezea  mataji raia huyo wa Serbia, ambaye sasa ameshinda mataji makubwa 19 katika mashindano haya.

Djokovich sasa anasalia na taji moja kufikia rekodi ya mataji 20 inayoshikiliwa na Roger Federer na Rafael Nadal.

Tsitsipas mwenye umri wa miaka 22  alikuwa na matumaini makubwa ya kushinda taji hilo baada ya kunyakua seti ya kwanza, na ya pili lakini Djokovich akaonekana kuimarika katika seti ya tatu.

Bingwa wa mashindano ya French Open kwa upande wa wanawake  Barbora Krejcikova kutoka Jamhuri ya Czech Juni 12 2021
Bingwa wa mashindano ya French Open kwa upande wa wanawake Barbora Krejcikova kutoka Jamhuri ya Czech Juni 12 2021 Christophe ARCHAMBAULT AFP

Kwa upande wa wanawake, Barbora Krejcikova kutoka Jamhuri ya Czech, aliibuka bingwa baada ya kumshinda Anastasia Pavlyuchenkova kuoka Urusi kwa seti za , 6-1, 2-6, 6-4, siku ya Jumamosi Juni 12 2021.

Hii ilikuwa fainali ya kwanza kati ya wachezaji hao wawili, na ilikuja baada ya magwiji wa mchezo huu Serena Williams kutoka Marekani kuondolewa katika hatua ya mwondoano huku Naomi Osaka akijiondoa.

Wachezaji wengine kama Simona Halep, Ashleigh Barty, Petra Kvitova walilazimika kuyaanga mashindano hayo kwa sababu ya majeraha.

Huu ni mwaka wa sita mfululizo kwa fainali ya wanawake, kumpata mshindi mpya.

  • 2016: Garbine Muguruza
  • 2017: Jelena Ostapenko
  • 2018: Simona Halep
  • 2019: Ashleigh Barty
  • 2020: Iga Swiatek
  • 2021: Krejcikova
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.