Pata taarifa kuu
FIFA-URUSI-KOMBE LA DUNIA 2018

Fahamu Kundi F, fainali ya kombe la dunia 2018

Kundi F:Hili ni kundi ambalo lina timu ambazo zina uwezo mkubwa wa kufika mbali katika michuano hii.Timu hizi ni pamoja na Ujerumani, Mexico, Sweden na Jamhuri ya Korea.Muhimu:- Mchuano wa ufunguzi utakuwa dhidi ya Mexico na Sweden, tarehe 17 mwezi Juni katika uwanja wa Luzhniki jijini Moscow.

Kundi la F
Kundi la F FIFA.COM
Matangazo ya kibiashara

Ujerumani:

Mchezaji wa Ujerumani
Mchezaji wa Ujerumani FIFA.COM

Kuelekea katika michuano hii ya kombe la dunia, Ujerumani ndio timu bora katika mchezo wa soka dunia.

Imewahi kushiriki mara 18. Mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 1934 na mwisho ilikuwa ni mwaka 2014.

Wameshinda taji hili mara nne, mwaka 1954, 1974, 1990 na 2014.

Imefanikiwa kufika katika hatua ya fainali mara nane, nusu fainali mara 13 katika historia ya michuano hii mikubwa duniani.

Kocha wa timu hii ni Joachim Low, ambaye amekuwa akiifunza Ujerumani tangu mwaka 2006 na mwaka 2014, aliisaidia nchi yake kunyakua kombe la dunia nchini Brazil.

Ni timu iliyo na wachezaji wazuri na wanaoweza kufunga mabao, lakini Toni Kroos mchezaji ambaye amewahi kuchezea Bayern Munich na Real Madrid anaonekana kuwa wa kuangaliwa sana.

Mexico

Timu ya taifa ya Mexico
Timu ya taifa ya Mexico FIFA.COM

Imecheza katika fainali 15 ya kombe la dunia kuanzia mara ya kwanza mwaka 1930.

Mwisho ilikuwa ni mwaka 2014 nchini Brazil.

Matokeo bora yalikuwa ni mwaka 1970 na 1986, ilipofika katika hatua ya robo fainali.

Kocha wa timu hii ni Juan Carlos Osorio raia wa Colombia , ambaye alianza kuifunza mwaka 2015, na kuisaidia timu yake kufuzu katika fainali hizi, kabla ya kumaliza michuano mitatu ya makundi.

Mchezaji anayeangaliwa sana katika kikosi hiki ni Javier Hernandez, ambaye aliongoza wenzake katika michuano ya kombe la dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini na Brazil 2014.

Anafahamika pia kama Chicharito na mashabiki wa soka duniani.

Sweden

Timu ya taifa ya soka ya Serbia
Timu ya taifa ya soka ya Serbia FIFA.COM

Nchi hii imeshiriki katika michuano hii mara 11. Mwaka wa kwanza ulikuwa ni mwaka 1934 na mwisho ilikuwa ni mwaka 2006.

Mwaka wa 1958, ilifanikiwa kumaliza ya pili katika michuano hii ya kombe la dunia. Huo ndio wakati pekee iliyowahi kufika katika hatua ya fainali.

Mbali na rekodi hiyo, imewahi pia kufika katika hatua ya nusu fainali mara nne.

Kocha Janne Andersson, ndio amekuwa nyuma ya mafanikio ya timu hii hadi katika hatua hii.

Aliweka historia kwa kuiondoa Italia katika mchuano muhimu wa kufuzu kucheza katika fainali hii.

Mchezaji wa kuangaliwa sana katika timu hii ni Marcus Berg, ambaye amejihirisha uwezo wake wa kufunga mabao na anachukua nafasi ya Zlatan Ibrahimovic ambaye amestaafu kuichezea timu ya taifa.

Jamhuri ya Korea

Timu ya taifa ya Korea
Timu ya taifa ya Korea FIFA.COM

Tangu kuanza kwa michuano ya kombe la dunia mwaka 1930, imefuzu mara tisa.

Mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 1954, lakini mara ya mwisho ilikuwa ni mwaka 2014.

Mwaka 2002 iliishangaza dunia kwa matokeo mazuri lakini iliiishia katika nafasi ya nne., wakati iliposhirikiana na Japan kuandaa fainali hii.

Kocha wa timu hii ni Shin Tae-Yong. Alipewa kibarua hiki tangu mwezi Julai mwaka 2017, baada ya kuondoka kwa Uli Stielike.

Licha ya ushindani mkali na mazingira magumu, alifanikiwa kuiongoza nchi yake katika michuano ya kombe la dunia.

Koo Jacheol ni miongoni mwa wachezaji wanaominikiwa kuwa wataongoza mashambulizi kuisaidia Taeguk Warriors katika fainali hii huko Urusi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.