Pata taarifa kuu
SOKA

Hugo Bross ni miongoni mwa Makocha 60 walioomba kazi ya kuifunza Bafana Bafana

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Cameroon Hugo Bross ni miongoni mwa makocha zaidi ya 60 walioomba kazi ya kuifunza timu ya taifa ya Afrika Kusini, Bafana Bafana.

Kocha wa timu ya taifa ya Cameroon Hugo Bross wakati wa michuano ya AFCON 2017
Kocha wa timu ya taifa ya Cameroon Hugo Bross wakati wa michuano ya AFCON 2017 ReutReuters/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Bross raia wa Ubelgiji ameomba kazi hiyo bada ya kuisaidia Cameroon kunyakua taji la mataifa bingwa barani Afrika AFCON mwezi huu nchini Gabon.

Mbali na Bross, makocha wengine walioomba kazi hiyo ni pamoja na Roberto Mancini na Giovanni Trapattoni wote kutoka Italia.

Wamjerumani Lothas Matthaus na Bernd Schuster pia wameomba kazi hiyo.

Makocha wengine wenye uzoefu mkubwa kama Hassan Shehata kutoka Misri na Samson Siasia kutoka Nigeria.

Shirikisho la soka nchini humo SAFA limesema wachezaji wa zamani Lucas Radebe na Benni McCarthy wameteuliwa katika Kamati maalum kuongoza kumpata kocha mpya.

Rais wa SAFA, Danny Jordaan amesema kuwa kocha mpya anatarajiwa kupatikana kufikia mwezi Machi ili kuanza maandalizi ya kufuzu katika kombe la dunia mwaka mwaka 2018 na kombe la mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2019 nchini Cameroon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.